Home LOCAL FAHALI WAWATAKA WAZAZI WASIMAMIE SEKTA ELIMU

FAHALI WAWATAKA WAZAZI WASIMAMIE SEKTA ELIMU


Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau akiongea na Wazazi wa Gongolamboto katika mahafali ya 17 Shule ya Msingi Ulongoni jana.
NA: HERI SHAABAN (ILALA )

MKURUGENZI wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau  amewataka wazazi kusingatia Elimu katika kufatilia Maendeleo ya watoto wao wasome mpaka kufikia vyuo Vikuu ili Serikali iweze kupata viongozi bora.

Neema Mchau aliyasema hayo katika mahafali ya 17 Shule ya Msingi Ulongoni ambapo alikuwa mgeni rasmi katika shule hiyo ambapo katika hotuba yake Neema aliwaasa Wazazi kuzingatia elimu kwa kuwaendeleza watoto waweze kusoma kumaliza darasa la saba sio mwisho wa Elimu kwani elimu aina mwisho watoto wana haki ya kupata elimu bora.
“Taifa lolote ili liweze kuendelea Wananchi wake lazima wapatiwe elimu bora sio bora Elimu nawaomba wazazi na jamii kwa ujumla marufuku tusiwapeleke watoto kwa ndugu baada kumaliza elimu ya Msingi kwani bado watoto wana haki ya kuendelea na elimu ya sekondari mpaka vyuo kumaliza elimu ya Msingi sio mwisho wa Elimu” alisema Neema Mchau

Neema alisema Dunia imeharibika katika kipindi cha Utandawazi kila mzazi ana jukumu la kulea mtoto wake mwenyewe  kwa Usalama wa Watoto wetu sio busara kumpa MTU mtoto wako akulelehe .

Neema aliwataka wazazi kuzingatia elimu na kuunga mkono juhudi za Serikali za elimu bila malipo katika kuwasimamia watoto waweze kusoma na kuwa viongozi wa baade.

Alisema katika sekta ya elimu inawaibua wataalam wengi wakiwemo wataalam, Madaktari, Mawaziri ,Waandisi, Wabunge ,Mawaziri kutokana na msingi bora wa elimu ambao jamii watawekea vizazi vyao.

Aidha Neema Mchau ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo alichangia viti 20 kwa ajili ya Walimu wa shule hiyo ya Msingi Ulongoni Wilaya ILALA.

Taasi ya Fahari Tuamke Maendeleo inamiliki Shule ya watoto Day Care Gongolamboto Wilaya ILALA .

Mwisho
Previous articleMABONDIA 20 KUZICHAPA OCTOBA 30,2021 DAR
Next articleNAIBU WAZIRI WA VIWANDA EXAUD KIGAHE ATOA NENO KWA WATUMISHI WA WMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here