Home SPORTS KIKOSI CHA SIMBA SASA KAMILI, WACHEZAJI WOTE KUREJEA KAMBINI LEO.

KIKOSI CHA SIMBA SASA KAMILI, WACHEZAJI WOTE KUREJEA KAMBINI LEO.

Na: Stella Kessy.

WACHEZAJI  wote walikuwa katika timu mbalimbali za taifa wanatarajia kuanza kurejea nchini  na kuingia kambini.

kwa mujibu wa  Kaimu Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba,Ezekiel Kamwaga amesema kuwa wachezaji  wa Tanzania wanatarajia kuingia  kambini  Jijini  Arusha leo.

“wachezaji wa Taifa stars   tayari wamemaliza  majukumu katika timu ya Taifa kwa awamu hii na wataingia kambini kujiunga na wenzao”anasema.

“Lakini pia kuna baadhi ya wachezaji  watawasili kesho lakini Taddeo Lwaga ambaye alikuwa Uganda tayari yupo nchini na ataondoka na wenzake wa stars kwenda kambini Arusha”ameongeza Kamwaga.

Kamwaga amewataja wachezaji waliokuwa katika timu ya Taifa ni Aishi  Manura,Shomari Kapombe,Mohamed Hussen,Muzamiru Yasin,Kennedy Juma,na Israel Mwenda wote Stars.

Wachezaji wengine ni  Maddie Kagere,(Rwanda)Perfect Chikwende,(Zimbabwe)Peter Banda (Malawi)Tadeo Lwaga (Uganda)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here