Home SPORTS FEI TOTO AIPA YANGA USHINDI

FEI TOTO AIPA YANGA USHINDI

 Na: Mwandishi wetu,Bukoba

KIKOSI cha Yanga leo wamibuka na ushindi 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo  wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa katika  Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera.

katika dakika za 24  kiungo  Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’  ameipa Yanga SC bao ambalo limedumu katika dakika 90 za mchezo.

Fei Toto amefunga bao hilo kwa shuti la mguu wa kushoto akimalizia mpira uliookolewa na kipa Issa Chalamanda kufuatia shuti la awali la mshambuliaji  Fiston Mayele.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, mabao ya mshambuliaji Vitalis Mayanga dakika ya tatu na 20 yameipa Polisi Tanzania ushindi wa 2-0 dhidi ya KMC Uwanja wa Black Rhino, Karatu mkoani Arusha.

Previous articleRAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU WA UINGEREZA MHE.TONY BLAIR IKULU CHAMWINO
Next articleDKT. GWAJIMA: SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA WEZESHI KWA NGOs NCHINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here