Home LOCAL FAMILIA NCHINI ZAASWA KUDUMISHA UPENDO WANANDOA WATAKIWA KUISHI MAISHA YA SALA

FAMILIA NCHINI ZAASWA KUDUMISHA UPENDO WANANDOA WATAKIWA KUISHI MAISHA YA SALA

 Na: Maiko Luoga, KILIMANJARO.

Familia za kikristo nchini zimeaswa kuishi kwa umoja, mshikamano na upendo zikitanguliza maombi yake kwa Mungu ili zijaliwe maisha mema siku zote.

Wito huo umetolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania na Dayosisi ya Tanga Dkt. Maimbo Mndolwa kwenye ibada ya kuombea ndoa za kikristo iliyofanyika Septemba 03/2021 kwenye Kanisa Anglikana Mtakatifu Mathia Hedaru wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

“Sheria za nchi zinaeleza wazi kuwa ndoa ni muunganiko wa hiari kati ya mume na mke walioamua kuishi pamoja, tafsiri hii inaendana na kanuni za Kanisa Anglikana Tanzania, hivyo tunamwomba Mungu awajalie wote waliopo kwenye ndoa waishi kwa upendo na amani” amesema Askofu Mndolwa.

Aidha Askofu Mndolwa amewaasa wanaume na wanawake walioamua kuingia kwenye ndoa kutimiza vyema majukumu yanayowapaswa kwa wenzi wao ili kuondokana na changamoto zisizo za lazima ambazo zinaweza kusababisha mifarakano ndani ya nyumba zao.

“Nitoe wito kila mmoja kumpenda mume au mke wake si kwa maneno tu bali kwa vitendo, wanawake ondoeni dhana ya kwamba zawadi lazima upewe wewe tu na mumeo bali wewe pia unao wajibu wa kumpa zawadi mumeo ili kuimarisha upendo” Askofu Mndolwa.

Baadhi ya washiriki wa ibada hiyo wamesema ujumbe huo unasaidia kurejesha upendo kwa wanandoa ambao wamefarakana na kuwarejesha pamoja huku wakidumu katika maisha ya sala.

Previous articleWIKI YA KAMPENI YA USAFI KUZINDULIWA MARA
Next articleBRELA YAWAHUDUMIA WANANCHI ZAIDI YA 200 NA KUTOA LESENI ZA BIASHARA PAPO KWA PAPO JIJINI DAR.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here