Home BUSINESS EQUITY BANK (T) NA PASS TRUST WAKUBALIANA DHAMANA ZA MIKOPO YA KILIMO...

EQUITY BANK (T) NA PASS TRUST WAKUBALIANA DHAMANA ZA MIKOPO YA KILIMO ILI KUONGEZA NEEMA KWA WAKULIMA NCHINI

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity (T) Robert Kiboti pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya PASS Trust Yohane Kaduma wakitia saini Mkataba wa Maridhiano (MOU) ambapo Taasisi ya PASS itatoa kiasi cha shilingi Bilioni 2.3 kama dhamana ya mikopo mbalimbali ya Kilimo ili kuongeza tija na uzalishaji.

DAR ES SALAAM.

Benki ya Equity (T) imetia saini Mkataba wa Makubaliano ya udhamini wa mikopo ya kilimo-Biashara na Taasisi ya PASS Trust, ili kurahisisha upatikanaji wa mikopo ya kilimo na hatimaye na kuongeza tija na uzalishaji.

Mkataba huo wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni moja ($1mn) ulisainiwa leo jijini Dar es Salaam na utawezesha kampuni ya PASS kutoa udhamini kwa wakopaji wa sekta ya kilimo ndani ya Benki ya Equity kwa kuanzia asilimia 20 mpaka 80. Maoneo yatakayo faidika na udhamini huo ni kilimo, uvuvi, ufugaji na shughuli zote katika minyonyoro ya thamani kwa sekta kilimo ikiwemo wajasiliamari, Taasisi ndogo za Fedha (MFIs) na vyama vya Ushirika.

Kilimo ni sekta muhimu kwa uchumi wa Tanzania, yenye kuchangia takribani asilimia 27% ya pato la taifa na kutoa zaidi ya 75% ya ajira zote nchini.

Akiongea katika hafla ya utiaji saini, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity (T) Robert Kiboti alisema: "Kilimo ni mhimili wa uchumi wetu. Katika Benki ya Equity, kilimo ni eneo linalopewa kipaumbele kikubwa. Tumeadhimia kuongeza wigo wetu wa kukopesha kwenye kilimo na kujiwekea lengo la mikopo ya kilimo kufika asilimia 30 ya jumla la mkopo yetu yote. 

Benki ya Equity, tunafurahi kuungana na washirika wetu wa PASS katika kuhakikisha kila mtu katika mnyororo wa thamani ya kilimo anaweza kupata fedha na mitaji inayohitajika katika kuongeza tija na kuwezesha uzalishaji bora. 

“Dhamira ya Benki ya Equity ni kuhakikisha kuwa anuwai za kilimo-SME zinapata suluhisho la kifedha katika hatua zote za mnyororo wa thamani, kutoka kwa uzalishaji hadi maeneo ya soko. Kwa hivyo, ni muhimu kwetu kuendelea kutoa fursa za kifedha ambazo yataweza upatikanaji wa mikopo nafuu na kwa urahisi zaidi na hivyo kuchangia mabadiliko chanya ya kilimo, uchumi, na maisha ya Watanzania kwa jumla, &quot” alibainisha.

Mkurugenzi Mtendaji wa PASS Trust, Yohane Kaduma, alipongeza ushirikiano ulioboreshwa kati ya PASS Trust na benki ya Equity, na kuwahamasisha wakulima na wafanyabishara kuchangamkia fursa hiyo adimu katika kuboresha kilimo nchini Tanzania. 

“Kuingia kwa benki ya Equity kwenye dhamana hii ya mikopo ya kilimo, kunaleta sasa jumla ya benki 14 zinazoshirikiana na PASS Trust katika kuwezesha ufikishaji wa mikopo nafuu ya kilimo kupitia mpango wa wetu wa dhamana ya PASS”

“Nichukue fursa hii kualika benki nyingi zaidi kujiunga na mfumo huu ili watanzania wengi zaidi wanaohusika katika biashara ya kilimo, waweze kupata mkopo na kuongeza uzalishaji. Kwa kuanzia, kampuni ya PASS Trust tumetoa takriban dola milioni moja (shilingi 2.3bn) kwa Benki ya Equity ili kufanikisha mpango huu mpya.” Alisema Bwana
Kaduma.

Katika makubaliano haya ya uendeshaji na benki ya Equity, PASS itatoa dhamana kati ya 20-60% ya mkopo (80% kwa wanawake) kwa Benki ya Equity ili kuongeza dhamana na kuwezesha upatikanaji mikopo kwa urahisi. Pia Miradi ya kilimo inayoongozwa na wanawake itafaidika na hadi dhamana ya 80% ya mkopo wa PASS. Mpaka sasa, zaidi ya wafanyabiashara milioni 1.7 wa biashara ya kilimo wameshafaidika na mpango wa dhamana ya mkopo wa PASS tangu ilipoanza mnamo mwaka 2000. Tangu mwaka 2017, PASS imeshasaidia upatikanaji wa mikopo ya kilimo inayofikia kiasi cha shilingi bilioni 6.7 kwa dhamana za Shilingi 2.6 bilioni chini ya mfumo huu wa dhamana mikopo ya mnyororo
wa kilimo.

Credit – Michuzi Blog.

(PICHA ZOTE NA: MICHUZI BLOG)


















Credit – Michuzi Blog.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here