Home LOCAL DKT. GWAJIMA AKUTANA NA UONGOZI WA HOSPITALI YA KANISA LAMBI DODOMA.

DKT. GWAJIMA AKUTANA NA UONGOZI WA HOSPITALI YA KANISA LAMBI DODOMA.

 
Na: WAMJW- Dom
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo amepokea ugeni wa uongozi kutoka Hospitali ya Kanisa Iambi Mkoani Singida ulioambatana na wawakilishi wa Watumishi wa Hospitali hiyo, ambao wamewasilisha taarifa ya changamoto mbali mbali zikiwemo stahiki za Watumishi katika Hospitali hiyo tangu mwaka 2018. Ikumbukwe, awali hospitali hii ilikuwa na mkataba na Wizara ya Afya na baadae Mei, 2021 ikahamishiwa kwenye Halmashauri husika.


Dkt. Gwajima amepokea taarifa hiyo na kuelekeza Kurugenzi ya Utawala ishirikiane na wadau wote husika ikiwemi Wataalamu kutoka OR TAMISEMI wajadili kitaalamu na kuwasilisha mapendekezo kwa Makatibu Wakuu na Mawaziri ili kumaliza changamoto hizo.

Aidha, Dkt. Gwajima ametoa siku 21 kwa Wataalamu hao kufanyia kazi maelekezo hayo.

Hata hivyo, Dkt. Gwajima anaomba Watumishi katika Hospitali hiyo kuwa watulivu na subira wakati changamoto hizo zikifanyiwa kazi.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here