Home LOCAL DKT. GWAJIMA AKUTANA NA UONGOZI WA HOSPITALI YA KANISA LAMBI DODOMA.

DKT. GWAJIMA AKUTANA NA UONGOZI WA HOSPITALI YA KANISA LAMBI DODOMA.

 
Na: WAMJW- Dom
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo amepokea ugeni wa uongozi kutoka Hospitali ya Kanisa Iambi Mkoani Singida ulioambatana na wawakilishi wa Watumishi wa Hospitali hiyo, ambao wamewasilisha taarifa ya changamoto mbali mbali zikiwemo stahiki za Watumishi katika Hospitali hiyo tangu mwaka 2018. Ikumbukwe, awali hospitali hii ilikuwa na mkataba na Wizara ya Afya na baadae Mei, 2021 ikahamishiwa kwenye Halmashauri husika.


Dkt. Gwajima amepokea taarifa hiyo na kuelekeza Kurugenzi ya Utawala ishirikiane na wadau wote husika ikiwemi Wataalamu kutoka OR TAMISEMI wajadili kitaalamu na kuwasilisha mapendekezo kwa Makatibu Wakuu na Mawaziri ili kumaliza changamoto hizo.

Aidha, Dkt. Gwajima ametoa siku 21 kwa Wataalamu hao kufanyia kazi maelekezo hayo.

Hata hivyo, Dkt. Gwajima anaomba Watumishi katika Hospitali hiyo kuwa watulivu na subira wakati changamoto hizo zikifanyiwa kazi.

Mwisho.

Previous articleMWENYEKITI WA CCM MHE. SAMIA SULUHU HASSAN, AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM
Next articleWAJUMBE WA KONGAMANO LA MISRI WAKUBALIANA KUKUZA UCHUMI LICHA YA COVID 19
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here