Home LOCAL DKT. GWAJIMA AFUNGUA KONGAMANO LA WAUGUZI KUTOKA NCHI 16 ZA AFRIKA MASHARIKI,...

DKT. GWAJIMA AFUNGUA KONGAMANO LA WAUGUZI KUTOKA NCHI 16 ZA AFRIKA MASHARIKI, KATI NA KUSINI ( ECSACON).

Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Dorothy Ngwajima akiongea na waandishi wa habari baada ya kufungua kongamano la kisayansi la 14 la wauguzi na wakunga kutoka nchi 16 za Afrika Mashariki, Kati na Kusini kongamano linaloendelea mkoani Arusha.

Mratibu wa kongamano la ECSACON Ibrahim Mgoo ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa umoja wa wauguzi na wakunga akiongea na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa kongamano lao linaloendelea mkoani Arusha.

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Zaidia ya wauguzi 300 kutoka nchi 16 za Afrika Mashariki, Kati na Kusini wamekutana Jijini Arusha katika kongamano la kisayansi la kimataifa la 14  la wauguzi (ECSACON) kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uuguzi na pamoja na kuweka mikakati ya namna bora ya kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi.

Akifungua kongamano hilo Waziri wa Afya Maendeleo ya ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt Dorothy Ngwajima amesema kuwa wauguzi hao wamekutana ili kuangalia maendeleo ya tasnia ya uuguzi na ukunga katika mustakabali wa kisayansi wanachangia vipi kwenye maendeleo ya jamii.

“Kama tunavyojua kwenye sekta ya afya karibu  nchi zote wauguzi ni sehemu kubwa ya watoa huduma katika huduma za afya hivyo ni lazima tuaangalie maslahi yao vizuri kwani na wao ni ishara  ya mwisho ya upendo ambao mwanadamu anaushuhudia kwani mtu anapoingia kwenye mtandao wa huduma za afya mtu anaye kutana nae mara nyingi ni  muuguzi,” amesema Dkt Ngwajima.

Amefafanua kuwa lazima wawaangalie wauguzi kuanzia masilahi yao, maendeleo ya taaluma na ustawi wao kwa ujumla  kwani mara nyingi maisha ya wagonjwa katika huduma za Afya yanakaa zaidi na wauguzi ikiwemo ICU ambapo muuguzi anaangaika kusaidiana na kudra za Mungu kuokoa maisha ya mgonjwa huyo.

Ameeleza kuwa kama waziri mwenye dhamana ya Àfya ya Tanzania  atakuwa msemaji wa umoja wao katika vikao mbalimbali vya mawaziri wa nchi hizo na kwa upande wa Tanzania atazifanyia kazi changamoto zinazowakabili  hasa  kuboresha maslahi yao kwani hayatoshi kwa ukubwa wa kazi wanaifanya na huku akitolea mfano wa ukonjwa WA UVIKO-19 ambao wauguzi wamekuwa mstari wa mbele kupambana nao.

Kwa upande wake mratibu wa kongamano hilo ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa umoja huo  Ibrahim Mgoo amesema kuwa kongamano hilo ni muhimu kwa wauguzi kwani huduma zinatakiwa kutolewa kisayansi ambapo pia kutakuwa na mada mbalimbali zitakazojadiliwa ikiwemo kuona ni namba gani wanaweza kusaidia kuondoa vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

“Tunataka tuone ni kwa namna gani tunaweza kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi lakini pia kuna  wajibu wa wananchi kuzingatia wanayoambiwa na wauguzi wanapoenda kliniki kwani wakiyafuata kwa usahihi vifo hivyo hawezi kutokea “Amesema Mgoo.

Aidha amesema kuwa mada nyingine watakayo jadili ni kuhusiana na ugojwa wa UVIKO-19 kwani kama wauguzi wao ndio wako mstari wa mbele kuangalia wagonjwa hivyo watapeana mbinu mpya za kuwahudumia wagonjwa pamoja na wao kujikinga.

Mkutano huo unafanyika kwa siku tatu Jijini humo ambapo mkutano uliopita ulifanyika mwaka 2018 nchini Kenya ikiwa ni mkutano wa 13.

Previous articleSIMBA QUEEN Vs LADY DOVES PATACHIMBIKA LEO.
Next articleRC MAKALLA: MARUFUKU MACHINGA KUFANYA BIASHARA KWENYE NJIA ZA WATEMBEA KWA MIGUU.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here