Home BUSINESS RC MAKALLA: MARUFUKU MACHINGA KUFANYA BIASHARA KWENYE NJIA ZA WATEMBEA KWA MIGUU.

RC MAKALLA: MARUFUKU MACHINGA KUFANYA BIASHARA KWENYE NJIA ZA WATEMBEA KWA MIGUU.

– Asema agizo hilo ni kwa Wafanyabiashara Mkoa mzima.
 
– Amtaka DC Ilala na Uongozi wa Machinga kuweka utaratibu mzuri kuwapanga Machinga Kariakoo.

– Awapo mbinu ya kufunga baadhi ya Mitaa Kariakoo kwaajili ya kufanya Biashara.

– Wamachinga wakiri kuingilia maeneo ya watembea kwa miguu na kuahidi kuhama.

– Aeleza dhamira yake ya kuboresha mandhari ya Dar es salaam.

Na: James Lyatuu, Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amepiga marufuku ufanyaji wa Biashara Kwenye maeneo hifadhi ya barabara zote za Mkoa huo baada ya utaratibu huo kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani na ongezeko la ajali.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo alipotembelea Soko la Kariakoo na kujionea Kero ya Ufanyaji biashara holela Kwenye maeneo ya watembea kwa miguu.

Kutokana na hilo RC Makalla amewaelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kufanya kikao na Wafanyabiashara hao Jumatatu ya September 13 na kuainisha maeneo ya kuwapeleka wote waliovamia hifadhi ya Barabara.

Aidha RC Makalla amewaelekeza Kuangalia utaratibu mzuri wa kufunga na kufungua baadhi ya Mitaa Kariakoo kwaajili ya kufanya biashara Kutokana na ufinyu wa maeneo ili Waweze kupata riziki.

Hata hivyo RC Makalla amesema kwa tathimini aliyofanya amebaini Hali ya Ufanyaji biashara holela Dar es salaam ipo kwa kiwango kikubwa na kuwanyima watembea miguu haki zao za msingi.


Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Manispaa zote za Mkoa huo kuweka Vibao vya kuzuia biashara Kwenye maeneo ya watembea kwa miguu.

Previous articleDKT. GWAJIMA AFUNGUA KONGAMANO LA WAUGUZI KUTOKA NCHI 16 ZA AFRIKA MASHARIKI, KATI NA KUSINI ( ECSACON).
Next articleWAZIRI MWIGULU AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA MISRI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here