Home LOCAL DIWANI SULTAN AMEZINDUA KAMPENI ALAMA ZA USALAMA BARABARANI

DIWANI SULTAN AMEZINDUA KAMPENI ALAMA ZA USALAMA BARABARANI

Diwani wa Kata ya Upanga Mashariki. Mwenyekiti wa Kamati za Mipango Miji na Mazingira Sultan Salim akiweka alama ya Punda Milia eneo la Shule ya Msingi SHAABAN Robart Leo September 12/2021 msaada uliotolewa na Wadau kwa ajili ya vivuko maeneo ya Shule Kata ya Upanga zikiwemo na za Usalama Barabarani(PICHA NA HERI SHAABAN).

Diwani wa Kata ya Upanga Mashariki. Mwenyekiti wa Kamati za Mipango Miji na Mazingira Sultan Salim akiweka alama ya Punda Milia eneo la Shule ya Msingi SHAABAN Robart Leo September 11/2021 msaada uliotolewa na Wadau kwa ajili ya vivuko maeneo ya Shule Kata ya Upanga zikiwemo na za Usalama Barabarani(PICHA NA HERI  SHAABAN).

DIWANI wa Upanga Mashariki Sultan Salim akizungumza na Afisa Tarura Upanga (PICHA NA HERI SHAABAN).
NA: HERI SHAABAN (ILALA).

DIWANI wa Upanga Mashariki Sultan Salim na Wadau wa Maendeleo wamezindua Kampeni za usalama Barabarani Kata ya Upanga Mashariki.

Kampeni hiyo ya Usalama Barabarani imezinduliwa leo shule ya SHAABAN ROBART Wilayani Ilala ambapo Kampuni ya RockyandGlo Enterprise imepewa tenda ya kuchora alama za Punda milia Barabara za Upanga kwa ajili ya  kupunguza ajali.

Akizindua Kampeni hiyo endelevu Maeneo  ya shule Diwani Sultan alisema anawapongeza wadau wa Upanga wakiwemo Shule ya SHAABAN Robart kwa kufanikisha kampeni hiyo  ambayo itakuwa ya Kata nzima.

“Nilipokuwa katika mkutano wa wananchi  walielezea kero kutokana kukosekana kwa alama za pundamilia maeneo ya shule Kata yangu imezungukwa na shule za Msingi na sekondari pia kuna kampuni ya kukamata magari imekuwa ikigeuza Kata ya Upanga Mashariki eneo la ATM kila wakati kukamata wapiga kula wake” alisema Sultan.
 
Sultan alisema Kata ya Upanga wameweka alama za usalama zinazotambulisha madereva wananchi wakikamatwa tena anakula sahani moja na hiyo Kampuni inayokamata gari bila kifuata taratibu.

Sultan alisema  Kata ya Upanga Mashariki ina shule saba za Msingi,sekondari tano na taasisi za Serikali na Vyuo.

Alisema jukumu la kuweka alama za Barabarani ni Tarura wadau wamebeba jukumu hilo kumsaidia Diwani wa Upanga Mashariki ili kumuondolea kero kwa wapiga kula wake

Ametaka TARURA iweke kipaumbele maeneo ya vikuko vya shule kuweka alama za Usalama Barabara ni ili kupunguza ajali kwa Wanafunzi.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here