Home ENTERTAINMENTS BONNY MWAITEJE,CHRISTOPHER MWAHANGILA NA UPENDO NKONE KUUNGURUMA TAMASHA LA SHUKURANI

BONNY MWAITEJE,CHRISTOPHER MWAHANGILA NA UPENDO NKONE KUUNGURUMA TAMASHA LA SHUKURANI


Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama ametangaza baadhi ya  waimbaji wa muziki wa injili watakaoshiriki katika tamasha la Kumshukuru Mungu linalitarajiwa kufanyika Oktoba 31, 2021 kwenye wanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake Kinondoni amewataja waimbaji hao kuwa ni Boniface Mwaiteje,Christopher Mwahangila na Mwanamama mwenye sauti nzito Upendo Nkone.

Ameongeza kuwa mbali ya waimbaji hao wakubwa nchini bado ataendelea kuwatangaza wanamuziki wengine wakati watakapokuwa wameweka sawa mambo kadhaa katika maandalizi ya tamasha hilo kubwa nchini. 

Ameongeza kuwa maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri na wanafanya mipango ya kuwa na waimbanji wakubwa wa muziki wa Injili kutoka nje ya nchi pia.

“Maandalizi ya tamasha la Kumshukuru mungu ni makubwa na tunatarajia kufanya tamasha kubwa sana na la kihistoria kwa kuwa muda mrefu wa zaidi ya miaka mitano tamasha la muziki wa injili hatujafanya hivyo ni wakati mzuri kwa watu wa mungu kujiandaa kulipokea tamasha hilo kubwa kwa mwaka huu,’.Amesema Msama.

 

Previous articleASKOFU MNDOLWA AONGOZA MAOMBI YA KUWAOMBEA WANAFUNZI WA MADARASA YA MITIHANI NCHINI.
Next articleBITEKO ATAKA MGAO WA MIFUKO YA MAWE YA DHAHABU UFANYIKE KWA SIKU NNE MFULULIZO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here