Home BUSINESS BITEKO ATAKA MGAO WA MIFUKO YA MAWE YA DHAHABU UFANYIKE KWA SIKU...

BITEKO ATAKA MGAO WA MIFUKO YA MAWE YA DHAHABU UFANYIKE KWA SIKU NNE MFULULIZO


Na: Cymon William, GEITA.

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika Kijiji cha Nyambogo Kata ya Nyakafulu Wilayani Mbogwe Mkoani Geita Wamelalamikia hali ya ucheleweshwaji wa mgao wa mifuko inayosadikiwa kuwa na dhahabu jambo linalopelekea kukosa fedha.

Wachimbaji hao wametoa lawama zao mbele ya Waziri wa madini katika mkutano uliofanyika Septemba 3 katika mgodi huo uliolenga kutatua kero za wachimbaji, ambapo walizitupia lawama ofisi za madini za mkoa mpya wa kimadini Mbogwe na kusema kuwa maofisa madini wamekua wakichelewesha mgao.

Akijibu hoja hiyo Waziri mwenye dhamana ya madini nchini Doto Biteko, amewaeleza wachimbaji hao kuwa kucheleweshwa kwa mgao katika machimbo hayo kunatokana na ofisi za madini katika Mkoa mpya wa kimadini Mbogwe kuzidiwa na majukumu kwani wanahudumia pia katika machimbo mengine yaliopo katika Wilaya ya Bukombe pamoja na halmashauri ya Nyang’wale.

Waziri Biteko aliwataka watumishi wa madini wa Mkoa wa Madini Mbogwe kugawa mifuko ya mawe yanayosadikiwa kuwa na dhahabu kwa siku nne mfululizo ili kupunguza msongamaono huo.

Previous articleBONNY MWAITEJE,CHRISTOPHER MWAHANGILA NA UPENDO NKONE KUUNGURUMA TAMASHA LA SHUKURANI
Next articleMWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI RUVUMA,
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here