Home LOCAL BENKI YA ABSA TANZANIA YAKABIDHI MSAADA WA VITANDA NA MAGODORO KWA SHULE...

BENKI YA ABSA TANZANIA YAKABIDHI MSAADA WA VITANDA NA MAGODORO KWA SHULE YA SEKONDARI WASICHANA AT TAAUN

 
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Melvin Saprapasen (kushoto), akimkabidhi vitanda na magodoro Mkurugenzi wa shule ya sekondari ya At – Taaun, Ali Betit kama sehemu ya majukumu ya benki kutoa kwa jamii kufuatia na uhitaji wa shule hiyo baada ya ajali ya moto kuteketeza thamani vikiwemo vitanda na magorodo hivi karibuni. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo, Morogoro hivi karibuni.
Mkuu wa Kitengo cha biashara kutoka Benki ya Absa Tanzania Melvin Saprapasen (wa pili kulia), akizungumza kabla hajakabidhi vitanda na magodoro kwa Mkurugenzi wa shule ya sekondari ya At – Taaun, Ali Betit (kulia kwake), kama sehemu ya majukumu ya benki kutoa kwa jamii kufuatia na uhitaji wa shule hiyo baada ya ajali ya moto kuteketeza thamani vikiwemo vitanda na magorodo. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo, Morogoro jana.

Meneja Huduma za Kijamii wa Benki ya Absa Tanzania, Hellen Siria (kushoto), akitoa salamu za pole kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya At – Taaun kufuatia ajali ya moto iliyoteketeza vitanda na magodoro ambapo benki hiyo imekabidhi vitanda 15 na magodoro ili kupunguza kero wanazokumbana nazo wanafunzi baada ya ajali hiyo. Ilikuwa ni katika hafla ya kukabidhi msaada huo shuleni hapo, mjini Morogoro, jana.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari wasichana ya At – Taaun iliyopo manispaa ya Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Benki ya Absa Tanzania na viongozi wa shule hiyo mara baada ya kupokea msaada wa vitanda na magodoro vilivyotolewa na Absa shuleni hapo jana.

Vitanda vilivyotolewa msaada na Benki ya Absa Tanzania kwa Shule ya Sekondari ya wasicha At – Taaun iliyopo Manispaa ya Morogoro baada uhitaji mkubwa kwa wanafunzi wa shule hiyo kutokana ajali ya moto iliyoteketeza mali za wanafunzi, vitanda na magodoro hivi karibuni. Picha hii imepigwa wakati wa makabidhiano ya vitanda hivyo shuleni hapo, Morogoro jana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here