Home SPORTS AZAM FC YAICHAPA HORSEED 3-1

AZAM FC YAICHAPA HORSEED 3-1

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Horseed ya Somalia katika mchezo wa kwanza Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Horseed waliwashitua wenyeji kwa bao la Ibrahim Nor dakika ya 22, kabla ya Azam FC kuzinduka kwa mabao ya Ayoub Lyanga dakika ya 32, Mkongo Idris Mbombo dakika ya 73 na Lusajo Mwaikenda dakika ya 78.

Timu hizo zitarudiana Septemba 18 hapo hapo Azam Complex na mshindi wa jumla atakutana na Pyramids ya Misri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here