Home SPORTS AZAM FC YAICHAPA HORSEED 3-1

AZAM FC YAICHAPA HORSEED 3-1

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Horseed ya Somalia katika mchezo wa kwanza Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Horseed waliwashitua wenyeji kwa bao la Ibrahim Nor dakika ya 22, kabla ya Azam FC kuzinduka kwa mabao ya Ayoub Lyanga dakika ya 32, Mkongo Idris Mbombo dakika ya 73 na Lusajo Mwaikenda dakika ya 78.

Timu hizo zitarudiana Septemba 18 hapo hapo Azam Complex na mshindi wa jumla atakutana na Pyramids ya Misri.
Previous articleRC SENYAMULE AFUNGUA SHULE BINAFSI YA ROYAL FAMILY GEITA
Next articleMAGAZETI YA LEO J.PILI SEPTEMBA 12-2021
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here