Home LOCAL AFISA ELIMU DAR AWATAKA WALIMU WAKUU KUANZISHA SKAUTI SHULENI

AFISA ELIMU DAR AWATAKA WALIMU WAKUU KUANZISHA SKAUTI SHULENI

NA:  HERI SHAABAN.

AFISA Elimu Mkoa Dar es Salaam Alhaj Abdul  Maulid amewataka Walimu Wakuu wa shule za  mkoa wa Dar es Salaam kuanzisha vijana wa skauti kila shule .

Afisa Elimu Alhaj Maulid alisema hayo Wilaya ya Ilala Leo katika kikao kazi  kwa ajili ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza 2022 kwa kwa Walimu wakuu wa shule za Serikali na binafsi.

“Naagiza kwa Walimu Wakuu wa shule katika mkoa huu kila shule kuanzisha skauti katika shule zenu na kuwajengea ukakamavu vijana  ” alisema Alhaj Maulid.

Pia aliwataka Walimu Wakuu wawatumie Vijana wa skauti vizuri     si kinyume chake.

Katika hatua nyingine Afisa Elimu  aliwataka Walimu Wakuu wa shule kuimarisha ulinzi SHULENI ikiwemo kujikinga na majanga ya ajali za moto ambazo zinatokea shuleni mara kwa mara.

Aliwapongeza kazi  ya Walimu ni wito hivyo wawe na nidhamu  na kuheshimu taratibu za kazi wakiwa watumishi.

Aliwataka wakuze taaluma na kuanzisha Michezo katika shule zao kwa ajili  ya kuwa anda wanafunzi katika michezo mbalimbali.

Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Dar es Salaam Mussa Ally alisema dhumuni la kikao hicho ni kikao cha kazi kwa ajili ya kuwandaa  kuwapokea wanafunzi wa mwaka 2022 ambapo katika Wilaya ya Ilala wamejipanga vizuri na Ofisi ya Mkurugenzi katika kusimamia ipasavyo.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here