Home BUSINESS WAZIRI MKUMBO ASAINI ITIFAKI YA KULINDA KAZI ZA WASANII NJE YA...

WAZIRI MKUMBO ASAINI ITIFAKI YA KULINDA KAZI ZA WASANII NJE YA NCHI.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (aliyeketi) akiwa katika picha yanpamoja na wajumbe wa Mkutano wa Wanachama wa Shirika la Haki miliki Afrika ( ARIPO) kutoka Tanzania Kutoka kushoto Andrew Shirima kutoka COSOTA, Mhe. Pauline Gekul Naibu Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo, Philemon Kilaka kutoka COSOTA, Denis Mzamilu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na Godfrey Nyaisa kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni ( BRELA).

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akifuatilia mjadala wa Mkutano Mkuu wa ARIPO kabla ya kusainiwa kwa itifaki ya Haki Miliki jijini Kampala, Uganda.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (watatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa ARIPO mara baada ya kusaini itifaki ya Haki Miliki jijini Kampala, Uganda.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) watatu kutoka kulia, akiwa katika picha ya pamoja na Mhe.Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt. Aziz Polnary Mlima (katikati) pamoja wa wajumbe wa mkutano mkuu wa Shirika la Haki miliki la Afrika (ARIPO) kutoka Tanzania akiwemo Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul (Mb), wanne kutoka kulia na Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Godfrey Nyaisa (kulia), mara baada ya kusainiwa kwa Itifaki ya Haki Miliki jijini Kampala, Uganda Agosti 27, 2021

KAMPALA, UGANDA.

Waziri wa Viwanda na Biasha Prof. Kitila Mkumbo  ameshiriki zoezi la utiaji saini itifaki ya usajili na ulinzi wa hiyari wa haki miliki utakaoleta tija na ufanisi kwa nchi wanachama na kulinda wasanii na kazi zao.


Zoezi hilo la utiaji saini limefanyika Jijini Kampala nchini Uganda ambapo Waziri Mkumbo pamoja na Mawaziri wengine wa nchi wanachama wa Shirika la Milki Bunifu ya Kanda ya Afrika (ARPO) walikutana kwaajili ya kujadili masuala ya Milki Bunifu kanda ya Afrika.


Akizungumza kabla ya kusainiwa kwa itifaki hiyo Waziri Prof. Mkumbo ameishukuru ARPO kwa kujadili na kufikia hatua ya kusaini  itifaki hiyo  ambayo imekuja katika kipindi ambacho jasho la wasanii limekuwa likipotea kwenye mikono ya maharamia.


“Ni vyema itifaki hii ikaanza kutekelezwa mara moja lengo kuu likiwa ni pamoja na kuwafikia wadau husika ambao ni waaanii na kuwapa fursa ya kuijua vizuri itifaki hii na hatimaye kujisajili na kuongeza kuwa hatupaswi kubaki serikalini na kwa wanachama wa ARPO pekee” akifafanua prof. mkumbo.


Ametoa wito kwa wasanii wote nchini kuchangamkia fursa hiyo itakayowawezesha kufikia soko la nchi zao na nchi wanachama wa ARPO kwa kupitia itifaki hiyo wasanii watakuwa na soko kubwa kwani kazi zao zitalindwa nje ya Tanzania kwa kufanya usajili mmoja.

Previous articleMWENYEKITI MARIATABU APANGA MIKAKATI YA KUFUNGUA VIWANDA VYA WANAWAKE BONYOKWA
Next articleHOSPITALI YA HARMONY YATOA KADI ZA BIMA YA AFYA BURE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here