Home Uncategorized MWENYEKITI MARIATABU APANGA MIKAKATI YA KUFUNGUA VIWANDA VYA WANAWAKE BONYOKWA

MWENYEKITI MARIATABU APANGA MIKAKATI YA KUFUNGUA VIWANDA VYA WANAWAKE BONYOKWA

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Bonyokwa Shaaban Mariatabu akizunguma na Wanawake na Vijana wa Bonyokwa Leo Agosti 28/2021 katika Kongamano la Wanawake piga lililoandaliwa na ofisi ya Serikali ya Mtaa wake (PICHA NA HERI SHABAN)

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bonyokwa Shabani Mariatabu akizungumza na Wanawake na vijana wa Bonyokwa Leo katika Kongamano la Wanawake piga kazi, lililoandaliwa na Serikali ya Mtaa wa Bonyokwa kwa kushirikiana na Joyce Kilia Wanawake live Leo Agosti 28/2021(kushoto)Joyce Kilia (PICHA NA HERI SHABAN).

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bonyokwa Shaaban Mariatabu akiongoza Wajasiriamali wa Bonyokwa Leo Agosti 28/2021 Katika Chakula cha mchana katika Kongamano la Wanawake piga kazi lililoandaliwa na Serikali ya Mtaa Bonyokwa (PICHA NA HERI SHABAN).

Mkurugenzi wa Hospitali wa HARMONY MEMORIAL POLICLINIC iliyopo Bonyokwa Wilaya Ilala Juliyan Mmary akizungumza wananchi wa Bonyokwa Dar es Salaam Jana , hospitali ya Harmony Memorial Policlinic inatoa huduma zote zikiwemo mama na mtoto (PICHA NA HERI SHABAN)

NA: HERI SHAABAN 
MWENYEKITI wa serikali ya Mtaa Bonyokwa Shaaban Mariatabu amepanga mikakati ya  kufungua  viwanda vidogo vidogo  vya Wanawake Bonyokwa.

Mwenyekiti Shaban Mariatabu alisema hayo katika Kongamano la Wanawake   piga kazi lililoandaliwa na Serikali ya Mtaa Bonyokwa kwa kushirikiana na Joyce Kilia wa WANAWAKE live .

“Nawaomba Wanawake wa Bonyokwa muunde majukwa ya kujikwamua KIUCHUMI yatakayowawezeha kupata mitaji mikubwa tufungue viwanda vidogo vidogo katika eneo letu la Bonyokwa ” alisema Mariatabu.

Mwenyekiti Mariatabu aliwataka Wanawake wa Bonyokwa kutumia fursa zilizopo ambazo zinatolewa na Serikali zitakazowawezesha kujikwamua KIUCHUMI kuacha maisha tegemezi.
 
“Nawaomba Wanawake wa Bonyokwa mjikwamue kiuchumi kwa kujishughulisha na biashara muweze kupata kipato kwa ajili ya kuendesha biashara zenu na kusomesha watoto ” alisema Shaban Mariatabu

Mariatabu alisema Serikali imewawezesha Wanawake katika mikopo ya asillimia kumi watumie fursa hiyo ya kukopa waweze kukuza mitaji yao wafikie malengo waweze kupata fedha za kusomesha watoto.

Aidha pia alisema Wanawake wa Bonyokwa watakapounda majukwaa ya kujikwamua  Kiuchumi wajenge mtandao wao wa biashara waweze kushirikiana na kujenga mahusiano .

Alisema halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inatoa mikopo kwa vikundi vya watu watano mpaka kumi ambao wanaminiana hivyo aliwataka Wanawake wa Bonyokwa ,Vijana na Watu wenye ulemavu kutumia fursa hiyo.

Kwa upande wake Joyce Kilia alisema mikakati yake kwa Wanawake wa Bonyokwa atawaweka pamoja katika masuala ya ndoa zao zisiyumbe waweze kufanya biashara zao bila kuvuruga mahusiano ya ndoa .

Joyce Kilia aliwataka Wanawake wa Bonyokwa kutumia fursa ya kuchukua mikopo vizuri na kabla kuchukua mikopo hiyo wajue wanakopa kwa lengo gani maana kuna Wanawake wengi wanachukua mikopo bila kupanga malengo sahihi .

Mwisho
Previous articleMAGAZETI YA LEO J.PILI AGOSTI 29-2021
Next articleWAZIRI MKUMBO ASAINI ITIFAKI YA KULINDA KAZI ZA WASANII NJE YA NCHI.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here