Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (aliyeketi) akiwa katika picha yanpamoja na wajumbe wa Mkutano wa Wanachama wa Shirika la Haki miliki Afrika ( ARIPO) kutoka Tanzania Kutoka kushoto Andrew Shirima kutoka COSOTA, Mhe. Pauline Gekul Naibu Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo, Philemon Kilaka kutoka COSOTA, Denis Mzamilu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na Godfrey Nyaisa kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni ( BRELA).
KAMPALA, UGANDA.
Waziri wa Viwanda na Biasha Prof. Kitila Mkumbo ameshiriki zoezi la utiaji saini itifaki ya usajili na ulinzi wa hiyari wa haki miliki utakaoleta tija na ufanisi kwa nchi wanachama na kulinda wasanii na kazi zao.
Zoezi hilo la utiaji saini limefanyika Jijini Kampala nchini Uganda ambapo Waziri Mkumbo pamoja na Mawaziri wengine wa nchi wanachama wa Shirika la Milki Bunifu ya Kanda ya Afrika (ARPO) walikutana kwaajili ya kujadili masuala ya Milki Bunifu kanda ya Afrika.
Akizungumza kabla ya kusainiwa kwa itifaki hiyo Waziri Prof. Mkumbo ameishukuru ARPO kwa kujadili na kufikia hatua ya kusaini itifaki hiyo ambayo imekuja katika kipindi ambacho jasho la wasanii limekuwa likipotea kwenye mikono ya maharamia.
“Ni vyema itifaki hii ikaanza kutekelezwa mara moja lengo kuu likiwa ni pamoja na kuwafikia wadau husika ambao ni waaanii na kuwapa fursa ya kuijua vizuri itifaki hii na hatimaye kujisajili na kuongeza kuwa hatupaswi kubaki serikalini na kwa wanachama wa ARPO pekee” akifafanua prof. mkumbo.
Ametoa wito kwa wasanii wote nchini kuchangamkia fursa hiyo itakayowawezesha kufikia soko la nchi zao na nchi wanachama wa ARPO kwa kupitia itifaki hiyo wasanii watakuwa na soko kubwa kwani kazi zao zitalindwa nje ya Tanzania kwa kufanya usajili mmoja.