Home BUSINESS WAZIRI MKUMBO AKABIDHI MPANGOKAZI KWA BODI YA USHAURI YA BRELA

WAZIRI MKUMBO AKABIDHI MPANGOKAZI KWA BODI YA USHAURI YA BRELA

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (kulia) akijadiliana jambo na Afisa MtendajiMkuu wa BRELA Godfrey Nyaisa (kushoto) alipokuwa akiizindua Bodi ya ushauri wa BRELA katika Ofisi za Wakala Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. KitilaMkumbo akizungumza na jopo la wana kamati aliyoiteua alipokutana nao kwenye ofisi za BRELA Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akimkabidhi moja ya wajumbe wa kamati hiyo vitabu vya miongozo mbalimbali itakayotakiwa kufanyiwakazi na Kamati hiyo.
(PICHA NA: HUGHES DUGILO).
 

Baadhi ya Watumishi wa BRELA waliokuwa wamehudhuria Hafla hiyo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)
Mwenyekiti wa Kamati teule ya Bodi ya Ushauri ya BRELA Prof. Neema Mori akimsikiliza Mhe. Waziri Prof. Kitila Mkumbo (hayumo pichani) alipokuwa akizungmza na Kamati hiyo.
(PICHA NA: HUGHES DUGILO).
 

Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Godfrey Nyaisa (kulia mwenye suti nyeusi) akiwa na Baadhi ya Wajumbe wa Bodi hiyo wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri Prof. Kitila Mkumbo (hayumo pichani) wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika katika Ofisi za BRELA Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)


Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa (kulia), akimkaribisha Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo, mara baada ya kuwasili katika ofisi kuu za Taasisi hiyo zilizopo Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam, Agosti 30, 2021 kwa shughuli ya uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya BRELA iliyoteuliwa hivi karibuni. (PICHA NA: CHISTINA NJOVU, BRELA)

DAR ES SALAAM. 

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo amekutana na bodi ya ushauri ya BRELA  na kuizindua rasmi ili majukumu yake.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa wajumbe hao kutoka BRELA Mhe. Mkumbo alisema majukumu makubwa katika bodi hiyo ni kumshauri na kusimamia menejimenti ya shirika lakini pia kuhakikisha kwamba wanaendelea kuboresha mazingira ili usajili wa biashara hapa Tanzania ufanyike bila vikwazo;

“Majukumu ya msingi ya bodi hii ni kunishauri kwenye mambo ya menejimenti ya  shirika letu kwasababu kwa sasa BRELA ni Taasisi muhimu sana katika mpango mkubwa wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan wa kuboresha mazingira ya biashara Tanzania”

Aidha Waziri Kitila alisema ni lazima biashara za Tanzania zinasajiliwe na pia zinarasimishwe ili watu waweze kulipa Kodi na kuajiri lakini pia biashara zao kukidhi kupata mikopo kutoka katika mabenki na Taasisi za kifedha;

“Tanzania tuna biashara nyingi ambazo siyo rasmi ,tunakadiria kwamba tuna takribani biashara ndogondogo na za kati Milioni 3 laki 7 katika hizo ni 4% pekeake ndizo ambazo zimesajiliwa sasa kurasimisha biashara kunanza na Biashara kusajiliwa na watu kuunda makampuni”

Waziri Kitila Mkumbo alisema kwa sasa biashara imeingia katika mtandao na kwa mazingira ya ugonjwa UVIKO -19 hawatarajii kuendelea kufanya biashara katika mazingira ya kawaida, hivyo tayari BRELA wapo katika mchakato wa kujiendesha kimtandao zaid.

Kutokana na BRELA kuwa na changamoto ya takwimu Waziri Kitila aliagiza baada ya miezi mitatu kuwe na Takwimu zote za msingi na ziwe na mfumo rahisi wa upatikanaji wa Takwimu hizo;

“Breala ina changamoto ya Takwimu, natarajia kwamba katika kipindi cha miezi mitatu ijayo tuwe na Takwimu zote za msingi na mtengeneze mfumo ambao ni rahisi kupata Takwimu za makampuni ya biashara Tanzania na leseni za biashara”

Mbali na hayo waziri Kitila alimaliza kwa kuiagiza bodi hiyo ikae haraka na wafanye uchambuzi kuhusu sheria kadhaa ikiwemo sheria mama ya makampuni ambayo wadau wamekua wakiilalamikia ikionekana baadhi ya vipengele kupitwa na wakati na kuona ni kiwango gani wanahitaji kufanya marekebisho katika sheria hiyo na kama inahitaji kuandikwa upya wamshauri aisogeze katika ngazi ya serikali na hatimaye ipelekwe bungeni.

Naye Prof. Neema Mori amemshukuru Waziri Kitila Mkumbo kwa kuwaamini wote waliopata nafasi ya kuingia katika bodi ya kuweza kumshauri na kuahidi kwa yote aliyowaagizia watatoa ushirikiano mkubwa kwa Menejimenti ya BRELA.

“Kwa maeneo sita ambayo Mhe. Waziri umeyatamka hapa tumeyapokea yote kwa mikono miwili na tunaahidi tutatoa ushirikiano mkubwa kwa wafanyakazi wote na tutakua katika nafasi ya kukushauri wewe Mhe. Waziri lakini pia menejimenti katika maeneo haya 6 ambayo yametajwa”

Ikumbukwe kuwa Kwa mujibu wa sheria ya wakala ya Serikali ya mwaka 1997 pamoja na marekebisho yake yaliyofanyika mwaka 2009 yanampa waziri wa Viwanda na Biashara mamlaka ya kuteua bodi ya ushauri ambayo itakuwa inamshauri kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Taasisi husika ambayo ni BRELA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here