Home LOCAL RC MAKALLA AKERWA NA MIGOGORO YA ARDHI KAWE NA KINONDONI DAR.

RC MAKALLA AKERWA NA MIGOGORO YA ARDHI KAWE NA KINONDONI DAR.

 

NA: KHERI SHAABAN.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amekerwa na migogoro ya ardhi ya Jimbo la Kawe na Kinondoni imechukua muda mrefu bila ufumbuzi wake .

Mkuu wa Mkoa Makalla aliyasema hayo katika siku ya kwanza ya  ziara yake kwa Mkoa wa Dar es Salaam  ya kutembelea majimbo ya Mkoa huo kwa lengo la  kusikiliza na kutatua kero  mbalimbali za wananchi

“Kata ya Kawe ni nyumbani kwangu nimeshawai kukaa leo nimeacha ofisi yangu nimeanza ziara ya kutatua kero za wananchi  katika Mkoa huu Jimbo la Kawe na Kinondoni linaongoza kwa mgogoro ya ardhi  “ alisema Makala.

Makalla alisema hajafurahishwa na migogoro hiyo ambayo migogoro mingine inachangiwa na Maafisa Ardhi wa Wilaya hiyo  wakiiipa Serikali hasara Chasimba Chasamba na Mabwepande amewataka wananchi kuandaa vielelezo vyao Mara baada ziara yake ya Mkoa kumalizika atakwenda na Waziri wa Ardhi William Lukuvi kutatua migogoro ya Ardhi .

Makalla alisema katika ziara hiyo amefurahishwa kumkuta Mbunge wa Jimbo la Kawe jimboni Josephat Ngwajima kusikiliza kero za wananchi wa Jimbo hilo.

Akizungumzia Maendeleo ya Jimbo la Kawe Mkuu wa Mkoa Makala alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Hassan Suluhu  imetenga shi bilioni 24 kwa ajili ya Barabara za Zege ,na za kiwango cha lami na Changalawe ,sekta ya maji shilingi bilioni 65  wananchi wataunganishiwa maji kutoka Ruvu .

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa Makalla amemwagiza Afisa TAKUKURU ,Afisa Ardhi na Mkuu wa Wilaya hiyo kuanzia kesho Agosti 31 /2021 kufatilia migogoro ya ardhi ya Jimbo hilo  kufuatia wananchi kuvunjiwa nyumba zao na mmiliki wa eneo hilo ambalo wananchi wanadai walilipa fedha benki milioni 15 kila mmoja bila kuwandikishiana .

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amewagiza Madiwani wa Mkoa Dar es Salaam ,Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Maafisa Watendaji wa Kata kufufua Ulinzi Shirikishi katika Kata zao na kuimalisha ulinzi na Usalama.

Kwa upande wake Mbunge wa Kawe Josepht Ngwajima alisema Jimbo la Kawe lina Kata kumi changamoto,Barabara, maji ya Dawasa,mafuriko ,vijana kukosa ajira wa Jimbo hilo.

Changamoto zingine Mbunge Ngwajima alisema Wananchi kubomolewa bila kulipwa,Mikopo ya Serikali kwa vikundi vya Wanawake na Watu wenye ulemavu pamoja na Wanafunzi kutembea umbali mrefu.

Mwisho

Previous articleWAZIRI MKUMBO AKABIDHI MPANGOKAZI KWA BODI YA USHAURI YA BRELA
Next articleMAJALIWA: SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here