Home BUSINESS TBL YATOA MALALAMIKO GHARAMA KUBWA MFUMO WA (ETS) KWA KAMATI YA BUNGE...

TBL YATOA MALALAMIKO GHARAMA KUBWA MFUMO WA (ETS) KWA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI, MEGA BEVAREGES WATAKA USHIRISHWAJI UPANDISHAJI KODI

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya bajeti wakuangalia uzalisha wa pombe kali aina ya K-VANT ukiendelea katika kiwanda cha Mega beverages mkoani Arusha.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya bajeti wakuangalia uzalisha ya kinywaji Cha bia aina ya Kilimanjaro ukiendelea katika kiwanda cha TBL.

Aliyeko mbele Ni Cliff Chilipachi Meneja uzalishaji wa kiwanda cha Mega beverages akiwaeleza kamati ya Bunge ya bajeti kuhusiana na uzalishaji wa pombe kali inayoendelea katika kiwanda hicho

NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imeieleza kamati ya Bunge ya bajeti kuwa mfumo wa teknolojia ya ETS umekuwa wa gharama kubwa ambapo kwa mwaka wanatumia zaidi ya bilioni 20 tofauti na awali ambapo walikuwa wakitumia shilingi bilioni 2 kwaajili ya utambuzi na kuhesabu  bidhaa wanazozizalisha.

Akiwasilisha changamoto hiyo mbele ya kamati ya Bunge mkurugenzi wa masuala ya ushirika na maendeleo endelevu wa TBL Messiya Mwangoka  amesema kuwa mfumo huo unaobandika stika na kuhesabu bidhaa wanazozalisha unamilikiwa na mtu binafsi tofauti na awali stika hizo zilikuwa zikibandikwa na TRA kwa gharama nafuu.

“Changamoto kubwa ya ETS ni gharama, inatugharimu fedha nyingi kwa bidhaa zetu kuhesabiwa tuu, tumewaonesha na tunamatumaini mtaenda kutoa ushauri kwa wizara husika ili tuweze kusaidika na hii bilioni 20 ni malipo ambayo tunamlipa mkandarasi ambaye anahusika na mfumo huu na sio serikali,” Alisema Mwangoka.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo Daniel Baran amesema kamati hiyo imesikia changamoto hizo  ambapo wao kama wazalishaji wameona ETS na baadae watakaa waone ni kwa namna gani wanaweza kuishauri Serikali ili nayo pamoja na wenye viwanda waweze kunufaika zaidi.

“Tumetembele TBL kujionea uzalishaji uliopo mahali hapa lakini kubwa Ni kujifunza kuhusu mfumo wa ETS  ambayo unatumika katika uzalisha na mfumo huu unaisaidia serikali kwa upande wa TRA kupata kiwango sahihi cha uzalishaji katika kiwanda,”Alisema Baran.

Amefafanua kuwa kwa bahati nzuri wenye kiwanda wamekiri wenyewe kuwa walishakaa na waziri wa fedha na mipango na kumweleza changamoto hiyo na Waziri akaunda kamati kwaajili hiyo hiyo watasubiri taarifa ya kamati ndipo waone ni namna gani wataweza kuishauri serikali.

Katika hatua nyingine kiwanda cha Mega beverages kinayojishughulisha na uzalishaji wa vinywaji vikali kimeiomba Serikali kuhakikisha kuwa upandishaji wa kodi unafuata sheria ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wadau wa kodi ili Serikali pamoja na walipa kodi kwa pamoja waweze kunufaika.

Ombi hilo limetolewa na meneja uzalishaji wa kiwanda hicho Chris Ndosi wakati walipotembelewa na kamati ya Bunge ya bajeti ambapo amesema kuwa kodi inapopanda bila wao kushirikishwa inakuwa ngumu kwao kwani wanahofia endapo watapandisha bei ya bidhaa ghafla itapelekea kupoteza wateja hali inayoweza kuathiri ustawi wa kiwanda.
 

Hata vivyo kamati hiyo kupitia mwenyekiti wake Daniel Baran imeahidi kuchukua changamoto hiyo ambapo wataenda kupitia na kuiwasilisha kwa Serikali.

Previous articleWATANZANIA TUSIPUUZE JITIHADA ZILIZOONYESHWA NA WACHEZAJI WETU KATIKA MASHINDANO YA OLIMPIKI 2020 NCHINI JAPAN.
Next articleSTEVE NYERERE AWATOLEA UVIVU WAPOTOTOSHAJI CHANJO YA UVIKO-19 MITANDAONI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here