Home ENTERTAINMENTS STEVE NYERERE AWATOLEA UVIVU WAPOTOTOSHAJI CHANJO YA UVIKO-19 MITANDAONI

STEVE NYERERE AWATOLEA UVIVU WAPOTOTOSHAJI CHANJO YA UVIKO-19 MITANDAONI


Mwenyekiti wa Taasisi ya UZALENDO KWANZA inayowaunganisha pamoja wasanii mbalimbali hapa nchini Steve Nyerere (katikati) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam. (kushoto) ni Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania Chiki Mchoma na (kulia) ni Msanii wa Maigizo Muogo Mchungu. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Mwenyekiti wa Taasisi ya UZALENDO KWANZA inayowaunganisha pamoja wasanii mbalimbali hapa nchini Steve Nyerere akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Mdau wa Sanaa na Michezo Asha Baraka (katikati) akizungumza kwenye mkutano huo juu ya kundi hilo la wasanii kuwahamasisha wanatanzania kupata chanjo (kushoto kwake) ni Mwenyekiti wa Taasisi ya UZALENDO KWANZA inayowaunganisha pamoja wasanii mbalimbali hapa nchini Steve Nyerere, na (kulia kwake) ni Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania Chiki Mchoma. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Sanii Maarufu wa Sanaa za Maigizo Muogo Mchungu akichangia jambo kwenye mkutano huo. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)
 

Mwenyekiti wa Taasisi ya UZALENDO KWANZA Steve Nyerere (kulia) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania Chiki Mchoma (kushoto) wakati wa mkutano huo. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)


Baadhi ya wasanii wa Sanaa za Maigizo wakishiriki Mkutano huo. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)


(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.

Watanzania hususani vijana wameshauriwa kutokubali kurubuniwa na maneno ya kwenye mitandao ya watu wanaoeneza upotoshaji juu ya chanjo inayoendelea kutolewa na Serikali kwa makundi ya watu mbalimbali hapa nchni.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Taasisi ya UZALENDO KWANZA inayowaunganisha pamoja wasanii mbalimbali hapa nchini Steve Nyerere katika mkutano wao na waandishi wa habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa wasanii hao kwa umoja wao wameamua kuunga mkono na kuhawamsisha wananchi wote likiwemo kundi kubwa la vijana kujitokeza kupata chanjo.

Steve Nyerere amebainisha kuwa wapo watu ambao wao walishapata chanjo nje ya nchi lakini wanatumika kuweka vitisho juu ya chanjo inayotolewa na hivyo kuitumia vibaya mitandao ya kijamii kupotosha umma wa watanzania huku wakijaribu kushawishi watu kuacha kuchanja.

“Sisi kama wana UZALENDO KWANZA tunaungana na Rais wetu mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuchanja, tunawaomba watanzania wenzetu na wasanii wenzetu wote tuchanje, tusisikilize maneno ya wanasiasa wanaotaka watu wasichanje sisi kama UZALENDO tunasema kuchanja ni hiyari, lakini kuna watu wao walishachanja nchi za nje hivyo wanatumia mitandao kuhamasisha watu wasichanje kwa namna moja ama nyingine tunawataka waache mara moja na kunyamaza kabisa wawaache watu watumie uhuru wao” Amesema Steve Nyerere.

Nakuongeza kuwa “tunahimiza vijana tusilishwe maneno lisitokee kundi la vijana wakalishwa embe ng’ongo wakazani ni tamu wajue mwishowe lina miba” alitahadharisha Steve, huku akiwasisitiza kuchanja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania Chiki Mchoma amesema kuwa ili kujenga Taifa lenye uchumi imara linahitaji watu wenye afya bora hivyo kwa kitendo cha Rais Samia kuonyesha mfano amelithibishia Taifa kuwa afya ni kitu cha msingi kwenye maisha ya mtu na kwamba wao kama wasanii watasimama na Mheshimiwa Rais kumuunga mkono  kuwahamasisha watanzania wote hasa vijana kupata chanjo ili kuendelea kuchapa kazi wakiendelea kujenga uchumi wa nchi yao.

”Tukichanja tutakuwa na huhakika wa afya zetu, tutakuwa na uhakika wa kufanya kazi vizuri na kuendelea kuujenga uchumi wa nchi yetu” ameongeza Chiki.

Nae mwanamama Asha Baraka amemshukuru Rais Samia kwa kuongoza zoezi la chanjo akisema kuwa huko ni kuwajali watanzania katika kuzilinda afya zao na kwamba ipo haja ya kila mtu kuona umuhimu wa kupata chanjo hiyo na kujihepusha na upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watu mitandaoni.

“kwanza kabisa nimshukuru sana Rais Samia kwa kutujali sisi watanzania kwa kutuletea hii chanjo na kuonesha mfano hivyo sisi tuko tayari na tutakuwa sambamba kama wasanii kumuunga mkono Rais wetu kwa kuwaendea Watanzania wote mikoani na vijijini kuwahamasisha kuchanja kwa hiyari yao wenyewe” amesema Asha Baraka.

Mkutano wa Taasisi hiyo ya UZALENDO KWANZA na waandishi wa habari umekuja ikiwa ni siku ya pili kwa muendelezo wa zoezi la Serikali kutoa Chanjo kwa hiyari kwa makundi maalum ya Wasanii, wanahabari, na wanamichezo lililoanza jana Agosti 12,2021 na kukamilika leo kwenye viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here