DAR ES SALAAM.
– Aamua kuongeza tena siku moja baada mwitikio kuwa mkubwa.
– Hadi Saa nne asubuhi tayari Wananchi 2,882 walikuwa wamepokea Chanjo.
– Kila aliepokea Chanjo apatiwa Cheti kinachotambulika kimataifa.
– Wananchi wampongeza RC Makalla kwa ubunifu wa kuwarahisishia kupata Chanjo.
Kufuatia mwitikio mkubwa wa Wananchi waliofurika Uwanja wa Uhuru kupata Chanjo ya Corona, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameamua kuongeza tena siku moja ya utoaji wa Chanjo ili kuhakikisha kila mwenye uhitaji anapata huduma.
RC Makalla ameongeza muda kufuatia Maombi ya Wananchi wa makundi mbalimbali walioomba muda uongezwe Kutokana na baadhi yao kushindwa kuhudhuria siku ya leo kwa sababu mbalimbali.
Aidha RC Makalla amesema adi kufikia majira ya saa nne Asubuhi kwa Mkoa huo tayari Wananchi 2,882 walikuwa wamechanjwa.
Hata hivyo RC Makalla amesema zoezi la leo limekuwa na mafanikio makubwa na kuendelea kuwasisitiza Wakuu wa Wilaya nao kuandaa zoezi Kama Hilo kwenye Wilaya zao ili kila mwenye uhitaji alate huduma hiyo.
Zoezi la utoaji wa Chanjo ya Corona kwa hiyari limeanza Leo uwanja wa Uhuru ikiwa ni maono ya RC Makalla alieamua kuwarahisishia Wananchi kupata huduma hiyo na litaendelea adi siku ya kesho Chini ya Watoa huduma zaidi ya 100 waliojidhatiti kuhakikisha kila anaejitokeza anapata huduma na kukabidhiwa cheti.