Home BUSINESS PROF.KITILA AITAKA TANTRADE KUWA KITUO SAHIHI CHA KUTOA TAARIFA

PROF.KITILA AITAKA TANTRADE KUWA KITUO SAHIHI CHA KUTOA TAARIFA

DAR ES SALAAM

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof Kitila Mkumbo (Mb.) ameitaka Mamlaka ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuwa kituo cha kibiashara kinachotoa taarifa, takwimu sahihi na huduma bora za kibiashara ndani na nje ya nchi ili kukuza na kuendeleza Biashara nchini.

Waziri Mkumbo aliyasema hayo katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANTRADE iliyofanyika Agosti 21, 2021, Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es salaam.

Akizindua Bodi hiyo, Prof Mkumbo aliitaka bodi hiyo kusimamia ipasavyo majukumu muhimu ya TANTRADE ikiwemo kuanzisha kanzi data yenye taarifa za kibiashara na kufanya utafiti ili kujua ni bidhaa gani zinazalishwa kwa wingi nchini, kuna upungufu wa bidhaa gani na bidhaa gani zinahitajika zaidi nje ya nchi.

“Nataka kuona TANTRADE inakuwa kimbilio kwa wanyabiashara katika kuwaunganisha wazalishaji, wasindikaji wafanyabiashara kutoka maeneo ya uzalishaji na walipo wtateja wa bidhaa zao  ndani na nje ya nchi kwa kutoa taarifa na takwimu sahihi pamoja na huduma bora za kibiashara”. Alisema Waziri Mkumbo.

Waziri Mkumbo pia ameitaka Bodi hiyo kuhakikisha TANTRADE inaongeza ubunifu katika matumizi ya mifumo mbalimbali ya kimtandao ya biashara inayolenga kuongeza upatikanaji wa taarifa mbalimbali za kibiashara kwa urahisi ili kuwezesha upatikanaji wa masoko ndani na nje ya nchi kwa bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini. 

Bodi hii pia inatakiwa kushirikiana na Taasisi  mbalimbali pamoja na sekta binafsi katika kuelimisha na  kuhamasisha uboreshaji wa bidhaa zinazozalishwa nchini,  upatikanaji wa masoko, uendeshaji wa biashara, kujenga uelewa juu ya usafirishaji  wa bidhaa hizo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati ili kufikia soko la ndani, kikanda na kimataifa. Alisema Prof. Mkumbo

Aidha, Prof. Mkumbo pia ameielekeza Bodi hiyo kutekeleza jukumu la msingi la Bodi katika kutengeneza mkakati wa kufikia malengo ya Taasisi na kusimamia utekelezaji wake kwa kutoa ushauri ndani na nje ya vikao vya Bodi, kuwa mtunza nidhamu wa Mkuu na Menejimenti ya Taasisi kwa niaba ya Mmiliki na kutoa  au kushauri katika kutatua changamoto za kimenejimenti huku ikizingatia kutokufanya kazi za menejimenti.

Previous articleWIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAENDESHA MAFUNZO YA KAIZEN KWA WAANDISHI WA HABARI NA WASANII DAR
Next articleRC MAKALLA ASHUHUDIA MAELFU YA WANANCHI WAMEJITOKEZA CHANJO YA CORONA UWANJA WA UHURU.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here