Home BUSINESS MAKATIBU WAKUU SMT NA SMZ WAKUTANA DAR ES SALAAM, WAJADILI CHANGAMOTO ZA...

MAKATIBU WAKUU SMT NA SMZ WAKUTANA DAR ES SALAAM, WAJADILI CHANGAMOTO ZA MUUNGANO

 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Athman Kattanga  (katikati) akiongoza Kikao cha pamoja cha Makatibu Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu – Dar es Salaam, leo tarehe 10/08/2021. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Ngelela Maganga na kulia ni Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais –SMZ Bw. Thabit Faina akimwakilisha pia Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa SMZ Mhandisi Zena Ahmed Said. Kikao hiki ni Maandalizi ya Kikao cha Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ ya Kushughulikia Masuala ya Muungano.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba na Bw. Christopher Kadio Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) wakifuatilia kikao cha pamoja na Makatibu Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu – Dar es Salaam.    
Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) wakiwa katika kikao cha pamoja kilichoketi katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu – Dar es Salaam leo tarehe 10/08/2021, ikiwa ni Maandalizi ya Kikao cha Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ ya kushughulikia Masuala ya Muungano.


Makatibu Wakuu kutoka Serikali Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wakiwa katika kikao cha pamoja na Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) kilichoketi katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu – Dar es Salaam leo tarehe 10/08/2021, ikiwa ni Maandalizi ya Kikao cha Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ ya kushughulikia Masuala ya Muungano.




LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here