Home LOCAL DKT. GWAJIMA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA FALME ZA KIARABU NCHINI TANZANIA.

DKT. GWAJIMA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA FALME ZA KIARABU NCHINI TANZANIA.

 

Na:WAMJW- DSM

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo amekutana na Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania (UAE) Mhe. Khalifa Abdulrahman Almarzouqi Kwenye ofisi ndogo za  wizara zilizopo jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao wamekubaliana kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika kupambana na magonjwa mbalimbali ikiwemo kudhibiti wimbi la tatu la ugonjwa wa Corona nchini.

Dkt. Gwajima amemhakikishia Balozi hiyo utayari wa Wizara yake  kushirikiana kwenye maswala yanayohusu uwekezaji kwa upande wa sekta ya afya pamoja na maendeleo  kitaifa. 

Previous articleMAKATIBU WAKUU SMT NA SMZ WAKUTANA DAR ES SALAAM, WAJADILI CHANGAMOTO ZA MUUNGANO
Next articleWATOTO WALIO CHINI YA MIAKA 5 ZAIDI YA MILIONI SITA WASAJILIWA RITA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here