Home LOCAL HOSPITALI YA HARMONY YATOA KADI ZA BIMA YA AFYA BURE

HOSPITALI YA HARMONY YATOA KADI ZA BIMA YA AFYA BURE

Mkurugenzi wa Hospitali wa  HARMONY MEMORIAL POLICLINIC iliyopo Bonyokwa Wilaya Ilala Juliyan  Mmary akiwa ameshika mmoja wa watoto mapacha wa Rose Kassim (32)(kushoto)Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa Bonyokwa SHAABAN Mariatabu na Diwani wa Bonyokwa Tumike Malilo wakiwa wamekumbatia mapacha wa Rose . 
(PICHA NA  HERI SHABAN

Mkurugenzi wa Hospitali wa HARMONY MEMORIAL POLICLINIC iliyopo Bonyokwa Wilaya Ilala Juliyan Mmary akizungumza wananchi wa Bonyokwa Dar es Salaam Jana , hospitali ya Harmony Memorial Policlinic inatoa huduma zote zikiwemo mama na mtoto (PICHA NA HERI SHABAN)

Na: HERI SHAABAN. 

HOSPTALI ya HARMONY MEMORIAL POLICLINIC itasaidia kumkatia bima za Matibabu za Watoto mapacha watatu waishio Bonyokwa Wilaya ya Ilala ambao wanaitaji msaada wa Serikali baaada kujifungua.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Harmony Memorial Policlinic Juliyan Mmary amechukua jukumu la kusaidia familia hiyo ya Mama Mapacha Watatu waliozaliwa na Rose Kassimu (35)kuwakatia kadi za Bima ya Afya ili wawe wanapatiwa matibabu katika vituo vya Afya kwa kipindi cha mwaka mzima . 
Juliana Mmary alisema msaada huo waliotoa kwa mtoto huyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusaidia jamii. 

“Hospitali yetu ya kisasa ya HARMONY MEMORIAL POLICLINIC ipo Kata ya Bonyokwa Wilaya ya Ilala na watoto hawa mapacha watatu wapo Bonyokwa ndio maana tumeguswa na hili kwa ajili ya kuisaidia familia hii waweze kuwalea watoto hawa wakue kesho wafike Ofisini kwetu na vielelezo vya utamburisho ikiwemo vyeti vya kuzaliwa ili waweze kupata bima ya afya‘alisema Juliana . 
Juliana Mmary aliwataka wananchi kukata Bima ya Afya kwa ajili ya matibabu ambapo pia katika hospitali watu wote wanapata matibabu wakiwemo wa kadi za bima ya afya wapo madaktari wa kisasa pia huduma za mama na mtoto wanatoa. 
Kwa upande wake Mama wa mapacha watatu Rose Kassimu (35)alisema kwa sasa ana watoto jumla saba wote wapo na kati ya watoto saba watoto mapacha amezaa mara mbili. 
Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here