Home ENTERTAINMENTS HAJI MANARA, LULU DIVA WAIBUKIA MISS TANGA 2021

HAJI MANARA, LULU DIVA WAIBUKIA MISS TANGA 2021

NA: MWANDISHI WETU.
ALIYE kuwa Msemaji wa timu ya Simba Haji Manara, anatarajiwa kuwa moja wa majaji wa shindano la miss Tanga Agost 28.

Akizungumza na ukurasa huu muandaaji wa shindano hilo Chuchu Hans amethibitisha uwepo wa Haji Manara kama mmoja wa majiji wa mchuano huo.

“Tuna endelea na maandalizi yana enda vizuri mpaka sasa namshukuru kaka yangu Manara kwa kukubali kuwa miongoni mwa majiji ambapo ata ambatana na msanii Lulu Diva,” anasema Chuchu.

Aliongeza kuwa kwa upande wa burudani jukwaa hilo litanogeshwa na mwanadada Rubby, pamoja na mchekeshaji Steve Nyerere ambao tayari wamesha thibitisha uwepo wao.

Fainali hiyo itafanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort  kiingilio ni VVIP 100000, VIP 50000 na kawaida 10000.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here