Home SPORTS TAASISI YA FAHARI YASAIDIA MIPIRA CLUB YA YONGWE FC

TAASISI YA FAHARI YASAIDIA MIPIRA CLUB YA YONGWE FC

Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau akizindua Bonanza LA Yongwe FC Chanika Wilaya ya Ilala Jana PICHA Na HERI SHAABAN).

Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau akikabidhi mpira kwa Kapteni wa Yongwe FC Chanika Dar es Salaam Jana (Katikati)Kocha wa Yongwe FC Abdalah Salehe Haule (PICHA NA HERI SHAABAN).

Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau akizungumza na Wachezaji wa Yongwe FC iliyopo Chanika Wilaya ya Ilala Dar es Salaam wakati wa kutambulisha club ya Yongwe na uzinduzi wake (PICHA NA HERI SHAABAN).

NA:  HERI SHAABAN (CHANIKA).

TAASISI ya Fahari Tuamke na Maendeleo imesaidia sekta ya michezo kwa kutoa msaada wa Mipira Club mpya ya Yongwe FC iliyopo Chanika Jimbo la Ukonga Wilayani Ilala.

Mipira hiyo iliyotolewa na Fahari Tuamke na Maendeleo Dar es Salaam jana  katika Bonanza la Michezo lililofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Yongwe ambapo club ya Yongwe FC ilitumia nafasi hiyo kutambulisha club yao ambayo imesajiliwa inajiandaa na ligi ngazi ya Wilaya Ilala .

Akizungumza wakati wa kukabidhi mipira hiyo Mkurugenzi wa TAASISI ya Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau alisema TAASISI ya Fahari inayomiliki Shule ya watoto Dar Care pia ina timu ya shule hiyo kwa ajili ya kuwaanda vijana katika michezo mbali mbali kwani michezo ni ajira ,michezo mahusiano na michezo ni afya.

Neema alisema  FAHARI Tuamke Maendeleo ni Taasisi ya kijamii pia inasaidia makundi mbali mbali ya kijamii ikiwemo sekta ya michezo pia ina Shule ya awali na sasa ipo katika mchakato wa kujenga Shule ya Msingi  kuanza darasa la Kwanza .

Alisema wameiwezesha klabu hiyo ili iweze  kukuza sekta michezo CHANIKA na Wilaya ya Ilala kwa ujumla.

“Taasisi yetu ya Fahari Tuamke Maendeleo leo imesaidia mipira miwili club hii ya YONGWE FC ili  iweze kushiriki mashindano ngazi ya Wilaya ya Ilala mwezi huu “alisema Neema.

Alipongeza Serikali ya Mtaa wa Yongwe,Ofisi ya Kata,na Diwani na Ofisi ya Kata kwa kuimalisha Kata ya Chanika na kufanikiwa timu kushiriki mashindano ya Wilaya.

Neema Mchau alimwagiza Kocha wa YONGWE FC kuanzisha timu nyingine ya Watoto wadogi kwa ajili ya kukuza vipaji vyao ili waweze kuandaa wachezaji bora.

wa upande wake Mratibu wa Yongwe FC Kocha wa Klabu hiyo  Abdalah Salehe Haule alipongeza klabu Fahari Tuamke Maendeleo kwa msaada huo wa vifaa vya michezo amewataka wadau wengine kuiga mfano huo kuwezesha sekta ya michezo.

Kocha Haule ameomba Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji Saady Kimji kuiwezesha klabu hiyo ili iweze kufikia  malengo yake na kuitangaza Chanika na Ilala kwa ujumla.

Aidha Haule aliomba Bonanza lingine lifanyike Baina ya Yongwe na Shule ya Fahari Tuamke Maendeleo.

Previous articleMAGAZETI YA LEO J.TATU AGOSTI 9-2021
Next articleHAJI MANARA, LULU DIVA WAIBUKIA MISS TANGA 2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here