Home SPORTS ARSENAL YAPOKEA KIPIGO KINGINE CHA 2-0 NA CHERSEA

ARSENAL YAPOKEA KIPIGO KINGINE CHA 2-0 NA CHERSEA

 

WENYEJI, Arsenal wamechapwa 2-0 na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates Jijini London.


Pongezi kwa beki wa kimataifa wa England, Reece James aliyemsetia Romelu Lukaku kufunga bao la kwanza dakika ya15, kabla ya yeye mwenyewe kufunga la pili dakika ya 35 akimalizia pasi ya Mason Mount.


Ni ushindi wa pili mfululizo kwa Chelsea katika mechi mbili za mwanzo za Ligi Kuu baada ya kuichapa 3-0 Crystal Palace na kipigo cha pili mfululizo kwa Arsenal ndani ya mechi mbili za mwanzo za msimu kufuatia kufungwa 2-0 na Brentford.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here