Home SPORTS ARSENAL YACHAPWA 5-0 MAN CITY

ARSENAL YACHAPWA 5-0 MAN CITY

MABINGWA watetezi, Manchester City wameendeleza ‘mauaji’ baada ya kuichapa Arsenal 5-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad, Manchester huo ukiwa ushindi wa pili katika mechi tatu, kufuatia kuchapwa 1-0 na Tottenham Hotspur na kushinda 5-0 dhidi ya Norwich City.

Katika mchezo huo ambao Arsenal ilimaliza pungufu baada ya Nahodha wake, Granit Xhaka kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 35 kwa kumchezea rafu Joao Cancelo, mabao ya Man City yamefungwa na Ilkay Gundogan dakika ya saba, Ferran Torres dakika ya 12 na 84, Gabriel Jesus dakika ya 43 na Rodri dakika ya 53.

Previous articleWIZARA YA AFYA YAPOKEA VIFAA VYA MILIONI 300
Next articleWAKULIMA WA MBAAZI TUNDURU WANEEMEKA NA MAUZO YA ZAO HILO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here