DAR ES SALAAM.
Waziri Lukuvi asema itafanya Dar es salaam Kuwa ya Kisasa zaidi.
RC Makalla asema wapo tayari kuipokea na kuzinduliwa muda wowote.
Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Mhe. William Lukuvi amesema Wizara hiyo tayari imekamilisha “Master plan” itakayokwenda kuboresha Jiji la Dar es salaam Kuwa la Kisasa ambapo amemuomba Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Amos Makalla kuandaa kikao Cha Wadau ili iweze kuzinduliwa.
Waziri Lukuvi amesema Master plan inayotumika Sasa ni ya Mwaka 1979 na imepitwa na wakati kwakuwa haiendani na Hali ya Sasa hivyo kupelekea Jiji kuonekana limejaa na hakuna nafasi ya Ujenzi lakini hii mpya itasaidia ongezeko la makazi kupitia Ujenzi wa Magorofa Kisasa zaidi.
Aidha Waziri Lukuvi amesema Wizara hiyo imefanya mazungumzo na Bank ya NMB na imekubali kuanza kutoa mkopo wa pamoja kwa Wakazi wa mtaa mmoja ili kutoa mkopo wa kusaidia zoezi la Upimaji wa Ardhi ili kuwezesha wananchi kupata hati za makazi.
Akizungumza wakati wa kikao kazi kilichojumuisha Viongozi wa Mkoa huo na watendaji wa Ardhi, Waziri Lukuvi amelekeza Mambo yafuatayo:-
-Ametaka utatuzi wa kero za Migogoro ya ardhi.
– Ameelekeza kuwepo kwa daftari la Migogoro ya ardhi* kwa kila Wilaya.
– Ametaka waliovamia Maeneo ya wazi kushughulikiwa.
– Amependekeza Maafisa watendaji wa Mitaa* kupewa jukumu la usimamizi wa Shughuli za Ujenzi na Mipango miji ndani ya Mitaa.
– Kampuni zilizolipwa na wananchi kwa kazi ya kufanya urasimishaji na Upimaji wa Ardhi na hawajakamilisha jukumu hilo kuchukuliwa hatua.
Miongoni mwa Migogoro sugu aliyogusia Waziri Lukuvi ipo Katika hatua nzuri ni Mgogoro wa Chasimba, Cha Tembo, Cha Chui, Nyakasange, Mabwepande na Gezaulole na Goba ambapo ametoa wito kwa Viongozi husika kuishughulikia pale ilipofikia.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amemshukuru Waziri Lukuvi na amewaelekeza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanashughulikia kero na Migogoro ya ardhi Katika maeneo yao.