Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha Mapinduzi CCM Iringa Vijijini wameahidi Kumuunga mkono Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa nguvu kutekeleza Ilani ya Uchaguzi wa 2020.
“Kwa kuwa ni mara ya kwanza kuwa na Rais Mwanamke Tanzania, sisi kama UWT Iringa Dc tunataka kumuunga mkono Mama Samia kwa kuhakikisha tunafanya kazi kwa nguvu zetu zote”
Akizungumza katika baraza la Uwt Iringa Vijijini, Mwenyekiti wa UWT Iringa Dc, Mama Lenah Hongole amesema wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Iringa Vijijini wako tayari kuendeleza kazi za utekelezaji wa Ilani kama ambavyo Chama Cha Mapinduzi kinaelekeza.
Mama Hongole amesema UWT Iringa Dc wameamua kuja na mkakati wa kuanzisha miradi mbalimbali kuanzia ngazi ya kata ili kukuza uchumi wa Mwanamke wa Iringa Vijijini.
Pia Mama Hongole amesema uanzishwaji wa miradi ya Kilimo, ufugaji na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwa wanawake wa Iringa Vijijini utaiwezesha Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Iringa Vijijini kujitegemea.
“Tutaanzisha mashamba ya miti na matunda, tutaanzisha viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali ambazo tutauza lengo ni kuwa huru na tuache utegemezi wa kiuchumi, pia tunampango wa kuanzisha ukumbi wetu utuingizie kipato”
Katika hatua nyingine wabunge wa Viti maalum mkoa wa Iringa wameonesha nia yao ya kusaidia maono ya UWT Iringa Dc ya kuwawezesha wanawake hao kiuchumi ili kuweza kujitegemea.
Kwa upande wake mbunge, Dkt Ritta Kabati ameeleza mkakati wake wa kuandaa andiko kwa kushirikiana na wataalam wa masuala ya biashara na viwanda ili kuanzisha viwanda vidogo kwa wanawake wa Mkoa wa Iringa.
“Nitaandaa andiko na wataalam wa mambo ya biashara na viwanda ili watushauri namna bora ya kuanzisha viwanda vidogo vya wanawake mkoa wa Iringa”
Nae mbunge Rose Tweve ameendelea kuelekeza nguvu zake katika kuhakikisha anawanyanyua wanawake kwa kuendeleza mikopo ya fedha kwa wanawake wa Iringa watokanao na UWT katika vikundi ili kuanzisha miradi mbalimbali.
“Mimi bado mpango wangu mkuu ni katika kuwawezesha wanawake mitaji, wanawake ndiyo nguzo yangu kuu hivyo lazima niwasaidie kiuchumi ili mjitegemee