Home LOCAL RC MAKALLA ASHUKURU VIONGOZI WA DINI KUOMBEA AMANI, ATAKA MAOMBI YA CORONA...

RC MAKALLA ASHUKURU VIONGOZI WA DINI KUOMBEA AMANI, ATAKA MAOMBI YA CORONA YAAMBATANE NA KUCHUKUA TAADHARI

 
 

DAR ES SALAAM.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo ameshiriki kongamano la Amani lililokwenda sambamba na Dua Maalumu ya Kuombea Viongozi sambamba na Maombi ya kuliombea Taifa dhidi ya Ugonjwa wa Corona ambapo ametoa wito kwa wananchi kulinda na kuitunza Amani.

Akizungumza wakati wa Kongamano hilo lililoandaliwa na Kituo Cha dua Cha Maalim Qassim, RC Makalla ametoa wito kwa wananchi kumuunga mkono Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ili aweze kutimiza matamanio yake ya kuboresha maisha ya Wananchi.

Aidha RC Makalla amewataka Wananchi kutokubali kugawanywa na mtu au kikundi Cha watu Wenye lengo la kuvuruga amani huku akiwataka kujihadhari na fitina.

Pamoja na hayo RC Makalla ameendelea kuwasisitiza Wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo hicho Maalim Qassim amemshukuru RC Makalla kwa kukubali ombi la ulezi wa Kituo hicho na ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali Katika Mambo mbalimba kwakuwa mbali na Kituo hicho kujihusisha na Dua pia kimekuwa walezi wa vituo vya watoto yatima.
Previous articleTCRA NA UCSAF WAPEWA MWEZI MMOJA KUJA NA MAPENDEKEZO KUTATUA CHANGAMOTO ZA MWINGILIANO WA MAWASILIANO MIPAKANI
Next articleUWT IRINGA VIJIJINI WAAHIDI KUMUUNGA MKONO MAMA SAMIA KWA KUFANYA KAZI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here