Home BUSINESS UBUNIFU WA WAJASIRIAMALI WA TWCC WAVUTIA WENGI MAONESHO YA SABASABA

UBUNIFU WA WAJASIRIAMALI WA TWCC WAVUTIA WENGI MAONESHO YA SABASABA

Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma Hamza (kushoto) akiwa na wageni waliofika kwenye Banda la Taasisi hiyo kupata kujionea namna Wajasiriamali hao wanavyofanya shughuli zao katika maonesho ya 45 ya kimataifa ya Biashara yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam,.
Afisa wa TWCC Cresencia Mbunda (kulia) akiwaelezea faida na fursa zinazopatikana mtu anapojiunga uanachama katika Taasisi hiyo kwa watu waliofika kwenye Banda lao wakati wa maonesho ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.

 
Wajasiriamali wa TWCC wakiendelea kutoa huduma ya kuelezea ubora wa Bidhaa wazazotengeneza kwa wananchi walifika kwenye maonesho hayo kwaajili ya kujifunza na kufanya manunuzi ya bidhaa za wajasiriamali hao.

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

WANANCHI wameendelea kujitokeza Kwa wingi kwenye Banda la Chama cha wanawake wajasiliamali Tanzania (TWCC) ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wajasiriamali na wafanybiashara kwa lengo la kutaka kujifunza masuala mbalimbali ya ujasaliamali.

Wananchi hao kupitia sikuku ya Sabasaba ambayo kila mwaka huadhimishwa Julai Saba wameonyesha kiu ya kutaka kujifunza na kutamani mafanikio ambayo tayari wengine wanayakata kutokana na kujikita kwenye ujasaliamali huo.

Akizungumza na  waandishi wa habari mmoja wa Wananchi  waliofika kwenye maonyesho hayo Sauli Willium amesema kuwa kabla ya kufika kwenye Banda hilo awali  walizunguka sana kutafuta Banda la TWCC  kwani kiu yao kubwa ilikuwa kufika kwenye Banda hilo ili kukutana na wajasiliamali na kupata uelewa zaidi

“Nimekuja na mke wangu ili tupate elimu ya ujasaliamali  lakini pia tujifunze namna ya kutengeneza unga wa mihogo Kwa ajili ya lishe na tumepata uelewa wa kutosha sana.kuhusu utengenezaji wake na sasa tumekwenda kujipanga .” amesema William

Amefafanua kuwa TWCC ni chama cha Wanawake wajasiliamali nchini lakini hainamaana kuwa wakinababa hawana nafasi ya kufanya ujasariamali na kujiunga kwenye Chama hicho nakwamba ndio maana ameambatana na mke wake ili baada ya kumalizika maonesho ya Sabasaba waanze utengenezaji wa unga wa lishe kupitia zao la muhogo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma Hamza akizungumzia ushiriki wao kwenye maonesho ya 45 ya Kimataifa amesema  kuwa anawaomba Watanzania wa rika zote  kusogea katika viwanja hivyo ambapo monesho yanaendelea hadi Julai 13 Mwaka huu.

Amesema wao kama TWCC wapo katika viwanja hivyo na Banda lao lipo karibu na jengo la Maliasili na Utalii  na linabeba wajasiriamali wanawake kutoka  Tanzania nzima hivyo na wanaonesho bidhaa mbalimbali za mikono na nyinginezo.

“Tunawakaribisha watu ambao wanataka kuwekeza na wanawake kwani kuina vitu vizuri  hivyo waje kushirikiana katika biashara na kitu chatofauti ambacho wanaweza kukipata vipo vingi mno kikubwa waje kwa wingi hapa “amesema

Ameongeza kuwa maonesho yanamuamko mkubwa na mamlaka husika wamejitahdi kufanya maandalizi mazuri na nakwamba msimu huu ni tofauti na misimu mingine kwani mwaka huu watu wamekuwa wengi toka siku ya kwanza yalipoanza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here