Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.
AFISA Biashara Mwandamizi Tantrade Norah Mishiri amewaomba wadau wajasiriamali kupitia maonesho ya kimataifa ya 45 ya sabasaba kuhudhuria kwenye mikutano ya ana Kwa ana B2B ili kupata maarifa ya kuendesha biashara zao.
Akizungumza na waandishi wa habari Norah amesema pamoja na mambo mengine wadau kwenye sekta ya ngozi wanajitahidi kutengeneza bidhaa hizo lakini changamoto kubwa ni kwa watumiaji na kwamba ifike mahala wananchi hususani watanzania kuunga jitihada zinazofanywa na wadau kwa kununua bidhaa zao ili kuwafanya waendelee kuzalisha bidhaa hizo kama vile Viatu vya Shuleni ,mabegi na vitu vinginevyo.
“Hapa nataka kusema kuna haja ya kuwaunga mkono wajasiriamali wetu hususani wadau wa bidhaa za ngozi kwani wanatengeneza bidhaa nzuri sana lakini tatizo ni kwenye masoko hivyo tuwaunge mkono.” Amesema.
Ameongeza kuwa hivi sasa inasemekana moja ya changamoto ni wimbi la bidhaa za ngozi kutoka nje ya nchi zinakwamisha soko la ndani Kwa watu wetu lakini wao kama Serikali hawawezi kuzuia uingizaji wa bidhaa hizo kwasababu bado hawajajua uzakishaji wa uhakika wa ndani.
Amesema kuwa kuna umuhimu wa kuwepo Kwa sera ambayo itarahisha kulitazama eneo la sekta ya bidhaa za ngozi hapa nchini nakufanya wadau kuwa katika hali nzuri ya kuwepo Kwa soko la uhakika hususani mashuleni.
Mikutano hiyo ya ana Kwa ana inaandaliwa na kuratibiwa na mamlaka ya biashara hapa nchini Tantrade Kwa lengo la kuwajengea uwezo wa wajasiriamali na wadau wengine wa biashara hapa nchini lakini pia ikiwamo kuunganisha Balozi za Tanzania katika kuangizia fursa za kibiashara kwenye nchi husika.
Mwisho.