Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Philip Mpango amelipongeza shirika la Madini Tanzania STAMICO kwa kuwa wabunifu na kuchukua tuzo ya ushindi wa jumla katika maonyesho ya kimataifa ya 45 ya biashara ya sabasaba ambayo yamefunguliwa rasmi leo kwenye viwanja vya maonyesho vya Mwalimu Julius Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa wilayani Tameke mkoanI Dar es salaam.
Dkt Mapango ametoa pongezi hizo leo wakati akihutubia wananchi waliojitokeza ,wajasiliamali pamoja na wafanyabiashara ambao wameshiriki maonyesho hayo ikiwa no pamoja na taasisi za serikali na makampuni binafsi
Amesema shirika la madini STAMICO limefanikiwa kuchukua tuzo hiyo kwakuwa wamekuwa wabunifu na kwakweli wamefanya vizuri lakini sio wao tu bali hata taasisi nyingine kama vile wadhamini wakuu wa maonyesho hayo Benki kuu ya Tanzania BoT, COSTECH pamoja na Benki ya biashara NBC ambao no miongoni mean wadhamini wa maonyesho hayo.
Naye Waziri wa Wizara ya madini Dotto Biteko akizungumza mara baada ya kutembelea banda la wizara ya madini hususani STAMICO Amesema kuwa ili kuweza kufanya vizuri katika sekta ya madini ni kutengeneza mfumo ambao utakuwa sera kwa bishara ya madini lengo lilies kudhibiti madini hayo na yajielekeze kwenye eneo husika kwa ajili ya mauzo,
Waziri Biteko ameongeza kuwa sekta ya madini iko vizuri na salama na matamanio yake nikuona sektra hiyo inachangia zaidi pato la taifa.
“Natamani kuona namba zinaongezeka zaidi tumetoka asilimia mbili hadi sasa tuko asilimia tano kwenye pato la taifa. na itakapofika miaka miaka mitatu ijayo tutakuwa mbali sana kwani tunamuamini Mungu katika hilo
Akizungumzia shirika hilo na mikakati mbalimbali ya kuwawezesha wadau kupitia sekta ya madini Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Dkt Venance Mwasse Amesema wanajisikia furaha kuchukua tuzo hiyo na imewapa chachu ya kuendelea kuwa bora nyakati zote kama wadau wanavyofahamu kuwa shirika hilo ndilo linashughulikia masuala ya madini nchini.
Ameongeza kuwa shirika la madini la taifa kama yalivyo mashirika mengine wameshiriki katika maonyesho hayo ili kuwaeleza watanzania shughuli mbalimbali zinazofanywa na ukizingatia kwamba shirika hilo ni muhimu sana na hivi sasa wamekuwa wakiwawezesha wachiambaji wadogo hususan viziwi katika kuhakikisha na wao wanashirika katika shughuli za madini.
Pia alizungumzia kuhusu mradi wa mgodi wa Kiwila wa makaa ya mawe ambao unatarajia kuzalisha nishati hiyo kwa matumizi ya majumbani na wamejipanga vizuri ili kuona mradi huo unawafikia watanzania na unakuwa tiba katika uharibufu wa mazingira wa ukataji wa miti kwa ajili ya kuni.
Amesema lengo la juhudi zinazofanywa na shirika nikuhakikisha wanawashika mkono wachimbaji wadogo na ndio maana wameaza na wachimbaji wadogo viziwi walioko kule mkoani Geita ili kuwafanya nao wanakuwa wachimbaji wakubwa hapo baadae.