Home SPORTS SIMBA SC YATWAA UBINGWA WA AZAM FEDERATION CUP (FA) YAICHAPA YANGA BAO...

SIMBA SC YATWAA UBINGWA WA AZAM FEDERATION CUP (FA) YAICHAPA YANGA BAO 1-0 KIGOMA

KIGOMA.

Timu ya Soka ya wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club imefanikiwa kunyakua ubingwa wa Kombe  la Azam Federation Cup (FA) kwa kuifunga timu ya Yanga goli 1-0 katika mchezo wa Fainali ya mashindano hayo uliopigwa kwenye dimba la Lake Tanganyika Mjini Kigoma.

Goli la Thadeo Rwanga lililopachikwa kambani mnamo dakika ya 80 kufuatia mpira wa kona iliyopigwa na kiungo Mshambuliaji Mzambia Cloutus Chama.

Timu ya Simba ambayo tayari imenyakua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara mara nne mfululizo, leo wameenelea kuandika historia nyingine kwa kunyakuwa ubingwa wa FA mara mbili mfululizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here