Home BUSINESS RC MONGELLA, TAHA WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO SEKTA YA HORTICULTURE ARUSHA.

RC MONGELLA, TAHA WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO SEKTA YA HORTICULTURE ARUSHA.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akiongoza mkutano wa majadiliano wa kuweka mikakati ya kukuza kilimo cha Horticulture kwa mkoa wa Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akiwa katika majadiliano ya kukuza sekta ya maua, mboga na matunda Mkoa wa Arusha na kushoto Ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAHA Dkt Jacqueline Mkindi.

Wadauo wa Sekta ya Maua, Mboga na matunda wakiwa katika kikao cha kujadili mikakati ya kukuza sekta hiyo mkoani Arusha.

Na: Namnyaki Kivuyo, ARUSHA.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amewataka wawekezaji kutoa taarifa wanapokutana na changamoto zozote kwani zina ufumbuzi na sio kuamua kufunga makampuni.

Mongela alitoa rai hiyo katika  mkutano wa wadau wawekezaji wa Sekta ya Horticulture uliofanyika mkoani Arusha kwa lengo la kujadili mikakati ya kukuza Sekta ya Maua, Mbogamboga, Mizizi  na Matunda ambapo alisema kuwa  watoe taarifa haraka na sio waamue kukaa kuchelewa kwani ikitokea hivyo ni wameamua  kumpa huyo anayewachelewesha ushirikiano.

Mongela alisema angalau wamepata fursa ya kuweza kujadiliana kwamba kwenye Horticulture waendaje na kuna dalili ya kufanikiwa hivyo wasichoke na Kama Serikali ya Mkoa wanaahidi watashirikiana nao wana kila sababu ya kushughulikia changamoto katika sekta hiyo hivyo wasisite kueleza kwani hawapendi mfanyabiashara yoyote akapata hasara.

Aidha ameitaka TAHA kushirikiana na Serikali ya Mkoa  na wadau wachache waweze kuwa na muongozo na kuweza  kuhesabu kila hatua wanayopiga maana yeye hapendi kwenda tuu bila kuangalia wapi wamefanikiwa wapi bado jambo ambalo  litasaidia  sekta hiyo kupata nguvu zaidi.

“lazima tuwe na wawezeshaji wazuri hiyo itasaidia kuona hata viwango vyetu kimataifa vinakuwa, TAHA anzeni kuongea na watu wanaotaka kuja kuwekeza watu wanaotaka kuja kufanya biashara ongeeni nao serikali ipo nyuma  yenu,”Alisema RC Mongela.

Alisema kuwa Sekta ya Horticulture ni eneo ambalo linaweza kuinua uchumi wa mkoa  hivyo wawe huru kwani wana wajibu na wameamua kufungua kituo cha biashara katika ofisi ya mkuu wa mkoa  kwa lengo la kutengeneze umoja ambao mtu akija anapata huduma zote sehemu moja ili waone ni kwa kiwango gani wanaweza kusaidia changamoto zinazokabili wafanyabiashara na wawekezaji ndani ya mkoa wa Arusha na kwenda kufanya kazi  ili wapate faida na serikali ipate faida kuliko kukaa kwenye urasimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi kilele inayojishughulisha na kilimo cha Horticulture cha maua, mboga mboga, matunda, viungo na mazao yatokanayo na mizizi (TAHA) Dkt Jacqueline Mkindi alisema kuwa  wamechukua muda mrefu kukubali kwamba mafanikio ya kiuchumi ya Taifa yanaweza kuletwa na kilimo cha Horticulture.

Alisema kuwa Horticulture Tanzania kabla ya Covid 19 ilikuwa inakuwa kwa asilimia 11 kwa mwaka ambapo  hivi sasa inakuwa kwa asilimia 7 huku Sekta hiyo ikiajiri watu wengi zaidi hasa wanawake na vijana.

“Tuna fursa nyingi lakini Tanzania inabidi wajipange kwani changamoto ya Kwanza inaanzia kwenye usafirishaji,suala la cold chain management ni kwenye viwanja vya ndege tuu lakini nyingine  wakiona contena la mboga mboga wanaliruhusu lipite haraka kama gari la wagonjwa kwasababu wanajua vilivyobebwa haviwezi kukaa kwenye joto vitaharibika lakini hapa kwetu Polisi hawajali magari yaliyobeba mazao hayo yanasimamishwa kila saa Kutoka mbeya hadi Arusha  kuna trafiki vituo 53,” Alieleza Dkt Mkindi

“Hadi mzigo ufike Airport mazao yameoza, lakini nchi nyingine wanaelewa na ndio mana wanapata faida kubwa kutokana na mazao tunatakiwa kubadilika  lori la barafu linafunguliwa zaidi ya mara 3 la sivyo watakuwa  wanawasindikiza wafanyabiashara wenzetu kwenye soko la kimataifa,” amesema.

Aidha aliiomba Serikali kuondoa madeni  yanayoidai mashamba 9 yaliyofungwa na kuwapa wawekezaji wapya kwani madeni hayo hayalipiki na kutengeneze kamati ya kushauri jinsi gani hayo mashamba yarudishwe na wawarudishe wawekezaji pamoja na kuandaa utaratibu wa kuchagua wawekezaji watakawekeza kwenye mashamba hayo.

Pia waliomba Serikali iangalie vigezo vya kuwapa wawekezaji wapya mashamba hayo ambapo walipendekeza waliohusika na hayo Mashamba awali  wasiruhusiwe kabisa kuingia, kama kuna ushirikiano ambazo zinahusika na uzalishaji wapewe kipaumbele, wasipokee  andiko la kuja kupanda katani kwenye mashamba hayo wanaiomba yarudi kwenye horticulture. Maua, mboga na kuendelea.

Aidha baadhi ya wadau wa horticulture, Gidion Ringo  kutoka kampuni ya Real IPM Tanzania LTD inayojishulisha na biological agent ili kusaidia wakulima wasitumie kemikali nyingi katika uzalishaji alisema bado kuna urasimu  wakati wa kuingiza na kutoa mizigo hasa mipakani na mkoa mmoja hadi mwingine kila siku wanaambiwa tozo tofauti  na hakuna mzigo uaingia hadi Arusha bila kutoa rushwa wa maafisa wa TRA na Polisi.

Mary Laizer kutoka Datiego Investment ambayo wanaanda green houses, kutengeneza dreep irrigation na mabwawa alisema mwamko kwa vijana katika kilimo bado ni mdogo hawajajengewa misingi kuwa kilimo kina manufaa, wanaona mkulima ni mtu wa chini lakini kuna kundi kubwa la vijana wanaoweza wanafanya kiwango cha kilimo  kikapanda hapa nchini.

Kwa upande wake Meneja wa TRA mkoa wa Arusha Kayobyo Majogoroa alisema kuwa mipakani  ni aibu kuona track ina vitu vya kuharibika alafu ikaisimisha kwa muda mrefu ambapo alieleza kuwa walienda wakajaribu kuwaelekeza maafisa wao lakini kama  kuna chochote kinakwama kwaajili ya TRA watoe taarifa wakati wa tukio na watashughulikia kwa wakati .

Alifafanua kuwa wataendelea kujenga mazingira ya kushirikiana ili kuhakikisha biashara zinakuwa na wao wanapata zaidi lakini aliwataka pia kufahamu kwamba miongoni mwa biashara ambazo zimerist kwenye biashara za TRA ni horticulture na waliokuwa wanaamini kuwa eneo hilo liko kwenye biashara kubwa 

“TRA ina wajibu wa kuwaelimisha lakini pia kuwasikiliza na wawaeleweshe vizuri kuhusiana na biashara zao na sio kuvutana tu kwenye suala la tozo tukae tuzungumze na kushauriana.

Naye kamanda wa polisi  mkoa wa Arusha ACP Jastin Masejo  alisema wana mchango mkubwa  kama polisi na mkoa wa Arusha ni sehemu yenye uchumi sana, watengeneze muunganiko kati yao na wadau wa sekta ili kutatua changamoto haraka pale zinapotokea.

“Nimeyachukua hayo yaliyolalamikiwa hasa ya kwenye vizuizi  na nitayafanyia kazi  na tangu nimekuja Arusha ni miezi mitatu lakini askari watatu wameshapoteza kazi kwaajili ya kwenda kinyume na maadili  kwahiyo mimi nipo makini nipeni tu taarifa inapotokea changamoto,” alisema ACP Masejo.

Previous articleWIZARA YA AFYA YATOA MWONGOZO WA UDHIBITI WA UGONJWA WA KORONA (UVIKO-19)
Next articleSIMBA SC YATWAA UBINGWA WA AZAM FEDERATION CUP (FA) YAICHAPA YANGA BAO 1-0 KIGOMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here