Katibu Tawala (RAS) wa Mkoa wa Mara, Albert Myovela (aliyevaa suti nyeusi) akipokea baraka kutoka kwa Baba Askofu Dkt Fredrick Shoo, baada ya kukabidhi mchango wa Sh milioni 1 uliotolewa na Mkuu wa Mkoa huo (RC) Ally Hapi, katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Kanisa hilo, Dayosisi ya Mkoa wa Mara jana. |
Baba Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dkt Fredrick Shoo (aliyevaa barakoa nyeupe) na Askofu KanisahiloDayosisi ya Mkoa wa Mara, Michael Adam muda mfupi kabla ya kuweka Jiwe la Msingi wa Jengo la Makao Makuu ya Dayosisi hiyo jana. |
Katibu Tawala (RAS) wa Mkoa huo, Albert Msovela pamoja na kuwasilisha mchango huo kwa niaba ya RC Hapi naye amechangia Sh 100,000(Laki moja) katika harambee ambayo imeongozwa na Baba Askofu wa KKKT, Dkt Fredrick Onael Shoo.
Jumla ya Sh milioni 54.6 taslimu zimekusanywa katika tukio hilo ambalo lililenga kukusanya Sh milioni 300.
Akizungumza baada ya harambee hiyo RAS Msovela ameahidi kuwa serikali itaendelea kutoa ushirikiano katika shughuli za maendeleo ya Kanisa hilo na kuomba liendelee kuombea amani nchini.
βPia napongeza jitihada za Kanisa katika kuhimiza na kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa korona, maana waumini wakiathiriwa hawatahudhuria Ibada wala kushiriki katika kuleta maendeleo ya Kanisa na taifa kwa ujumla,β amesema RAS Msovela.
Naye Askofu Dkt Shoo ameshukuru Serikali ya Mkoa huo kwamba imejipambanua kuwa ni waumini wa kutoa ushirikiano kwa vitendo, siyo maneno.