Home LOCAL MAONESHO YA 16 YA ELIMU YA JUU YALIYOANZA LEO KUFUNGULIWA RASMI KESHO...

MAONESHO YA 16 YA ELIMU YA JUU YALIYOANZA LEO KUFUNGULIWA RASMI KESHO JULAI 27,2021 DSM

Muonekano wa Banda la TCU kwenye maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza leo na kufunguliwa rasmi kesho Julai 27,2021 katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.

Afisa Ithibati Mkuu wa TCU Petro Mugandila (wa pili kushoto) akiwa na Katibu Muktasi wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Joyce Lema (kulia) wakitoa Elimu juu ya huduma za TCU kwenye Banda lao wakati wa Maonesho hayo yaliyoanza leo kwenye viwanja vya mnazi mmoja na kufunguliwa rasmi kesho Julai 27,2021

Afisa Ithibati Mkuu wa TCU Petro Mugandila (kulia) akiendelea na zoezi la kutoa Elimu kwa wanafunzi waliotembelea Banda la TCU kwenye maoneshohayo.

Afisa Udhibiti Ubora wa TCU Bahati Dyegula (Kushoto) akitoa maelezo ya namna Tume hiyo inavyotekeleza jukumu lake kwenye maeneo mbalimbali likiwemo la udhibiti ubora wa Vyuo Vikuu mbalimbali ili kuhakikisha wanafunzi wao wanapata Elimu bora na yenye Viwango vinavyohitajika.

Maafisa wa Chuo cha Biashara (CBE) wakiwa kwenye Banda lao katika Maonesho ya 16 ya TCU yanayotarajiwa kufunguliwa rasmi kesho Julai 27,2021 katika viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam. (wa kwanza kulia) ni Afisa kutoka Idara ya Masoko wa Chuo hicho na Mkufunzi Eunice Nyange, (katikati) ni Afaisa kutoka Idara ya Masoko Neema Kitonka, na (wa kwanza kushoto) ni Afisa Mitihani wa Chuo hicho Patrobas Chaulo.
 

Afisa Udahili wa Chuo cha CBE Godson Kyense (kushoto) akiendelea na zoezi la udahili kwa wanafunzi waliojitokeza kwenye Banda lao kwaajili ya kutaka kujiunga na Chuo hicho.

 
 

Picha Mbalimbali za washiriki wa maonesho hayo kutoka kwenye Taasisis na vyuo mbalimbali hapa nchini.

Previous articleRC HAPI ACHANGIA SH.MILIONI MOJA HARAMBEE UJENZI WA MAKAO MAKUU YA KKKT MARA.
Next articleTOFAUTI BEI ZA BIDHAA KATI YA KENYA NA TANZANIA MPAKA WA SIRARI CHANZO CHA MAGENDO MKOANI MARA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here