Home LOCAL RAIS.MHE.SAMIA KUSHIRIKI MDAHARO WA KUMBUKIZI YA MAISHA YA HAYATI BENJAMINI MKAPA

RAIS.MHE.SAMIA KUSHIRIKI MDAHARO WA KUMBUKIZI YA MAISHA YA HAYATI BENJAMINI MKAPA

Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi ya Benjamini Mkapa Foundation, Dkt.Hellen Senkoro akizungumza na waandishi wa habari leo  Jijini Dar es Salaam akitoa taarifa ya kuwepo  kwa mdaharo wa kumbukizi ya maisha ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamini Mkapa.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

NA: EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mdaharo wa kumbukizi ya maisha ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamini William Mkapa utakaofanyika siku ya tarehe 14 Julai mwaka huu Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Mdaharo huo umeandaliwa na taasisi ya Benjamini Mkapa Foundation kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam,Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Dkt.Hellen Senkoro amesema kuwa mdaharo huo ni sehemu ya kuenzi mchango wa hayati Benjamini Mkapa kwenye taifa hili, Afrika na Duniani, ambao utafanyika chini ya kauli mbiu isemayo “HAYATI BENJAMINI MKAPA:MWAKA MMOJA TANGU  ATUTOKE, TUNAYAKUMBUKA MAISHA YAKE, TUNAENZI URITHI WAKE”.

Amesema viongozi mashuhuriwanaotarajia kushiriki kupitia uwepo wao binafsi au kwa njia ya mtandao ni pamoja na aliyekuwa Rais wa 42 wa Marekani Mhe.Bill Clinton, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe.Tonny Blair, aliyekuwa Rais wa Nigeria Mhe.Olegesun Obasanjo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa wa kupambana na UKIMWI (UNAIDS) Bi.Winnie Byanyima ambao wote kwa pamoja watatoa salaam zao kwa njia ya video wakielezea walivyomfahamu Hayati Benjamini Mkapa katika kushirikiana nae katika kazi mbalimbali za kuleta maendeleo  Duniani hususan katika Bara Afrika na nchini Tanzania.

“Viongozi wengine wa kitaifa ambao  watakaohudhuria mdaharo  huo ni pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe.Dkt.Hussein Mwinyi,Viongozi wakuu  wa Serikali, Marais na Viongozi Wastaafu  kutoka Tanzania Bara na Visiwani, Mabalozi  wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa hapa nchini, Wakuu wa  Taasisi mbalimbali za Umma pamoja na Asasi za kiraia na viongozi wa dini”. Amesema Dkt.Senkoro.

Aidha Dkt.Senkoro amesema licha ya kuwa na mdaharo pia Rais Mhe.Samia atazindua mfuko maalumu wa Taasisi “Endowment Fund”.Mfuko huo  unaanzishwa chini ya Taasisi ya Benjamini Mkapa, una lengo la kuongeza chachu katika kuimarisha huduma za afya nchini.

 

Previous articleMILIONI 381 ZAWALETEA FURAHA WAKAZI WA KIJIJI CHA LIUGHAI WILAYANI LUDEWA.
Next articleMISS TANZANIA AIPONGEZA STAMICO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here