Home ENTERTAINMENTS MISS TANZANIA AIPONGEZA STAMICO.

MISS TANZANIA AIPONGEZA STAMICO.

DAR ES SALAAM.
Miss Tanzania 2020 Bi. Rose Manfere leo ametembelea banda la  STAMICO na kuipongeza kwa kazi nzuri inayofanya kwa kipindi chote cha maonesho ya 77 katika kuelimisha umma hasa kuhusu uchakataji na uongezaji thamani katika Madini, matumizi ya mkaa wa mbadala wa Rafiki Briquettes.

Akiongea kuhusu Maonesho ya sabasaba  amesema amefurahia sana kufika katika banda bora la STAMICO na kupata elimu juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na  STAMICO.

Amesema ni mara chache Sana elimu hii hutolewa kwa wananchi wa kawaida hivyo imekuwa na tija kubwa kwake kwa kuwa amefahamu hatua zote jinsi Madini yanavyopatikana.

Amepongeza kwa Ubunifu mkubwa uliotumika kwenye muonekano wa banda na katika kutangaza bidhaa mbalimbali za Shirika na husani Mkaa mbadala na hasa jinsi utakavyosaidia  kina mama wakati wa kuutumia jikoni.

Ametoa wito kwa watanzania kutumia Maonesho haya ya Sabasaba ili wapate kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na  Wizara ya Madini na Taasisi zake.
Previous articleRAIS.MHE.SAMIA KUSHIRIKI MDAHARO WA KUMBUKIZI YA MAISHA YA HAYATI BENJAMINI MKAPA
Next articleWATAALAM CHUKUENI VIPIMO, MSIANGALIE PEKEE KWENYE TATIZO LA UPUMUAJI ILI KUMTAMBUA MGONJWA WA CORONA -DKT. GODWIN MOLLELl

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here