Home BUSINESS Rais Dkt.Mwinyi azindua Zanzibar Golden Tulip Airport Hotel

Rais Dkt.Mwinyi azindua Zanzibar Golden Tulip Airport Hotel

 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akisalimiana na Mwenyekiti wa Makapuni ya Royal Group Bw. Mohammed Eaza Daramsi alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Kisasa ya Golden Tulip Zanzibar Airport, (katikati) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uwezeshaji Uchumi Zanzibar Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akiwa na Viongozi wa Serikali na Wamiliki wa Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar Airport, wakimsubiri mgeni rasmin Rais swa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa ajili ya kuifungua Hoteli hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Wawekezaji wa Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar Airport, ilioko jirani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipiga makofi baada ya kumaliza kuweka jiwe la msingi la ufunguzi wa Hoteli hiyo ya Kisasa ya Golden Tulip Zanzibar Airport jirani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuifungua rasmi Hoteli ya Kisasa ya Kitalii ya Golden Tulip Zanzibar Airport jirani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Jijini Zanzibar (kulia kwake) Mwenyekiti wa Makampuni ya Royal Group.Bw. Mohammed Raza Daramsi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Zanzibar.Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Royal Group Bw.Hassan Mohammed Raza.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakitembelea hoteli hiyo baada ya kuifungua rasmin wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Royal Group Bw.Hassan Mohammed Raza akitowa maelezo kwa mgeni rasmi. wakati akitembelea.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakitembelea hoteli hiyo baada ya kuifungua rasmin wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Royal Group Bw.Hassan Mohammed Raza akitowa maelezo kwa mgeni rasmi. Wakati akitembelea.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakitembelea Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar Airport jirani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Jijini Zanzibar, baada ya kuifungua Hoteli hiyo akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Royal Group Bw.Hassan Mohammed Raza.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Royal Group Bw. Hassan Mohammed Raza akitowa maelezo wakati akitembelea Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar Airport jirani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Jijini Zanzibar, baada ya kuifungua rasmi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakitembelea Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar Airport jirani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Jijini Zanzibar, baada ya kuifungua Hoteli hiyo akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Royal Group Bw.Hassan Mohammed Raza.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakielekea katika eneo maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi katika hafla ya ufunguzi wa Hoteli ya Kitalii ya Golden Tulip Zanzibar Airport jirani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Jijini Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Royal Group Bw. Hassan Mohammed Raza akizungumza na kutowa maelezo ya kitaalum ya ujenzi wa Hoteli hiyo ya Kitalii ya Golden Tulip Zanzibar Airport, wakati wa hafla ya ufunguzi wake rasmin uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Hussein Ali Mwinyi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwezeshaji Zanzibar Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli ya Kisasa ya Utalii ya Golden Tulip Zanzibar Airport, kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi kuzungumza na Wananchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi katika ufunguzi wa Hoteli ya Kisasa ya Kitalii ya Golden Tulip Zanzibar Airport, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya hoteli hiyo.









Waalikwaka waliohudhuria uzinduzi wa Hoteli ya Kitalii ya Golden Tulip iliyopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar wakifuatilia kwa makini na kusikiliza taarifa zilizotolewa katika sherehe ya ufunguzi wa hoteli hiyo leo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka watendaji wa Serikali kuwa mstari wa mbele katika utoaji wa huduma pamoja na misaada ili kuhakikisha matatizo yanayowakabili Wawekezaji yanapungua.
Dkt. Mwinyi ametoa wito huo leo katika ufunguzi wa Hoteli ya kitalii ya Nyota tano ya ‘Zanzibar Golden Tulip Airport Hotel’ iliyopo pembezoni mwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume jijini Zanzibar.
Amesema, Serikali imekuja na Sera ya Kuvutia Wawekezaji, hivyo mtendaji yeyote atakaekwenda kinyume au kukwamisha azma hiyo atalazimika kuwa nje ya Serikali.
Amesema, hatua ya serikali ya kuleta mabadiliko kiutendaji katika kipindi kifupi kijacho, inalenga kuvutia wawekezaji , na kubaiinisha kuwa wawekezaji wanahitaji utendaji wa kisasa.
Aidha, Dkt. Mwinyi amesema tayari Serikali imeanza kuchukua hatua, husuan kwa taasisi zinazotoa huduma kwa wananchi, pamoja na kuhakikisha utendaji katika sekta binafsi unahamia Serikalini.
Rais Dkt. Mwinyi alisema Serikali ya Awamu ya Nane kwa kushirikiana na sekta binafsi inahakikisha inaweka mazingira mazuri ya uwekezaji, hivyo akatumia fursa hiyo kuwahimiza wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kujitokeza bila khofu kushirikiana an Serikalii katika kupanga na kutekeleza miradi kwa njia ya PPP.

Utaratibu huu umekuwa ukitumika sasa na kupendwa na wawekezaji katika nchi mbalimbali kwa njia ya Public Private Partneship – PPP,” amesema.

Amesema, ujenzi wa hoteli hiyo unakwenda sambamba na dhamira ya serikali ya kuimarisha sekta ya Utalii, usafirishaji pamoja na biashara.
Amesema, kwa kipindi kirefu wasafiri wengi wanaotaka kusafiri nyakati za asubuhi wamekuwa wkaisumbuka kupata malazi ya uhakika karibu na kwianja cha ndege kama ilivyo katika viwanja vyengine vya Kimataifa.
Alisema hoteli hiyo hivi sas aitaqweza kutoa huduma hizo, ikiwa na miumbombinu muhimu na ya kisasa itakayowawezesha kupata huduma muhimju zinazotolewa na mashirika ya Ndege hapa nchini na hivyo kuongeza idadi ya wageni.
Aidha, Dk. Mwinyi alionyesha kufarijika kwake na kusema mbali ya kuwepo changamoto mbali katika sekta ya utalii zinazotokana na kuzuka kwa maradhi ya Corona Covid – 19, bado wawekezaji wa sekta hizo kwa kushiirikiana na Serikali wameendelea kuwekeza mitaji mikubwa hapa nchini.
Katika hatua nyengine Dk. Mwinyi alitoa pongezi kwa Kamapuni ya Estim Construction kwa umakini na umahiri mkubwa katika ujenzi wa Jengo hilo, ambapo pamoja na mambo mbali mbali lina kumbi kubwa za kupendeza kwa ajili ya mikutano ya Kitaifa na Kimataifa.
Mapema, Waziri wa Nchi, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhan Soraga alisema Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya Uwekezaji kwa kuimarisha sheria hatua aliyobainisha inalengo la kufungua milango ya Uwekezaji ili kuhakikisha Zanzibar inakuwa kituo muhimu cha Uwekezaji katika Ukanda wa Nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Nae, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Sharif Ali Sharif alisema Mradi wa ujenzi wa Hoteli ya kisasa ulithibitishwa na Mamlaka hiyo (ZIPA) ukiwa na mtaji wa makisio wa Dola za Kimarekani milioni 7.
Alisema kuwa mradi huu ambao utafanya biashara zake kwa jina la Golden Tulip Inn Airport Hotel, mpaka sasa umeshawekeza zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 9, ikiwa sawa na ongezeko la asilimia 28 ya makisio ya mtaji wa awali ambapo hadi sasa utekelezaji wa mradi huo umeshafikia zaidi ya wastani wa asilimia 90.
Aliongeza kuwa Kampuni ya Royal Group of Companies tayari imewekeza miradi sita kupitia ZIPA katika sekta ya ukarimu, huduma za uwanja wa ndege, huduma za biashara na viwanda ambazo zinatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya uwekezaji nchini, kukuza uchumi na kutengeneza ajira hususan kwa vijana.
Sharif alisema kuwa mradi huo umeingiza dhana mpya ya utalii ijulikanayo kwa jina la “MICE” yenye maana ya Utalii wa Mikutano, Vivutio, Mikutano ya Kimataifa na Maonyesho ambapo dhana hiyo itasaidia sana kupanua wigo wa sekta ya utalii na kuacha kutegemea pekee utalii wa hoteli za fukwe.
Akieleza hali ya uwekezaji kwa ujumla kupitia Mamlaka hiyo, Sharif alisema kuwa tangu kuanza kazi kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya Nane mwezi Novemba 2020 hadi kufikia Julai 2021, Mamlaka imefanikiwa kusajili jumla ya miradi 50 yenye jumla ya mitaji ya Dola za Kimarekeni milioni 321.
Alisema kuwa hali hiyo inaonyesha kuwepo kwa mwamko mkubwa wa wawekezaji wanaokuja kuwekeza Zanzibar kutokana na Mikakati ya Rais Dk. Mwinyi ya kuimarisha na kuvutia uwekezaji nchini.
Mapema, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya “Royal Group of Companies” Hassan Mohammed Raza alisema kuwa jengo hilo liliwekewa jiwe la msingi Januari 4, 2020 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaaliwa baada ya ujenzi kuanza rasmi mnamo Februari mwaka 2019.
Alisema kuwa, Hoteli hiyo itakuwa na hadhi ya Nyota tano yenye vyumba 60 ambapo lengo na madhumuni ya ujenzi huo karibu na uwanja wa ndege utasaidia malazi karibu na uwanja wa ndege hususan kwa wasafiri wa ndege za usiku sana au alfajiri, wafanyakazi wa ndege na abiria ambao ndege zao zinachelewa kuruka au safari zilizofutwa.
Alisema kuwa hoteli hiyo itakuwa na kumbi tatu za mikutano wenye uwezo wa kuchukua watu 40, 200 na mwengine utakuwa na uwezo wa kuchukua watu 1,000 ambapo pia, itakuwa na mikahawa, bwawa la wazi la kuogelea na sehemu ya kucheza watoto.
Alisema kuwa jumla ya Dola za Kimarekanimilioni 9 zimewekezwa hadi kukamilika ujenzi wa hoteli na ukumbi mkubwa wa mikutano ambapo matarajio ni kuendelea na uwekezaji zaidi na kufikia katiya Dola milioni 13 hadi 15.
Aidha, alingeza kuwa hoteli hiyo imejengwawa kuzingatia masharti na ubora unaohitajika kwa hoteli ya uwanja wa ndege ambapo miongoni mwao ni pamoja na vioo vya madirisha vya kuzuia kelele za ndege.
Previous articleSHANTA GOLD YAPONGEZWA KUSIMAMIA LOCAL CONTENT
Next articleNAIBU WAZIRI WA ELIMU AYAFUNGA RASMI MAONESHO YA 16 YA VYUO VYA ELIMU YA JUU LEO JULAI 31,2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here