Home BUSINESS PURA YAJIPANGA KUTANUA WIGO WA KUWAFIKIA WADAU WA SEKTA YA MAFUTA NA...

PURA YAJIPANGA KUTANUA WIGO WA KUWAFIKIA WADAU WA SEKTA YA MAFUTA NA GESI NCHINI.


Na: Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM.

DAR ES SALAAM.

Mamlaka ya udhibiti wa Mkondo wa juu wa Petroli (PURA) cha imewataka wadau mbalimbali kutembelea Banda lao ili kupata maelezo na kujifunza namna ambavyo Mamlaka hiyo yenye dhamana ya kusimamia na kudhibiti shughuli za uchimbaji wa Mafuta wa Mkondo wa juu inavyotekeleza shughuli zake.

Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wazawa na Uhusishwaji wa Wadau PURA Charles Nyangi ameyasema hayo wakati wa maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika Katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa mkondo wa juu ni hatua ya utafutaji na mamlaka hiyo iliazishwa chini ya sheria yamwaka 2015 na moja ya majukumu miliyopewa ni kuhakikisha wadawa wanshirikiwa ili kufahamu mambo ya mafuta na gesi .

Nyangi ameyasema hayo  kwenye maonesho ya kimataifa ya 45 ya sabasaba ambayo yanaendelea katika viwanja vya mwalimu nyerere barabara ya kilwa temeke jijini Dar es salaam ambapo amesema moja ya kazi ni kuhakikisha wazawa wanashirikia moja kwa moja katika kufanya biashara moja kwa moja na makampuni husika.

Pia amesema jukumu lingine ni kuhakikisha wazawa wanawekeza katika Sekta ya mafuta na gesi hivyo wananchi wajitokeze kwenye viwanja  vya sabasaba ili kupata uelewa na maelekezo kuhusu shirika hilo la PURA na kuona fursa zilizopo.

“Tupo kwenye viwanja vya sabasaba hapa kwenye maonyesho nifursa kwa wadau wafanyabishara kujifunza na kujua moja ya kazi na majukumu ya shirika letu la Pura kwani wataklaamu wetu wapo na watatoa maelezo mazuri.’’amesema nyangi.

Nae Magambo Samweli amesema kuwa wadau wafike kwenye banda lao ili kupata histori kuhusu Gesi ambapo inahistoria kubwa na kufikia miaka hii ambapo makampuni sasa yanaweza kugundua upatikanaji wa gesi kwenye maeneo yetu hususani mkoani mtwara.

Amesema kuwa kazi ya pura sasa nikuhakikisha wayasimamia makampuni hayo ili kuweza kuleta tija kwenye sekta hiyo ambapo serikali waliona kuna umuhimu wa kuwepo shirika hilo ili kuweza kusimamia mambo mbalimbali yanayotokana na kazi ya shirika hilo la pura hivyo wapo kwenye maonyesho hayo.

Mwisho.

 

 

 

 

Previous articleTCRA YAJIDHATITI KUWEZESHA UKUAJI WA UCHUMI KIDIJITALI
Next articleKAMATI YA UCHAGUZI WA (NaCoNGO) YARIDISHWA NA MCHAKATO WA UCHAZI NGAZI YA MIKOA NA WILAYA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here