Home LOCAL KAMATI YA UCHAGUZI WA (NaCoNGO) YARIDISHWA NA MCHAKATO WA UCHAZI NGAZI YA...

KAMATI YA UCHAGUZI WA (NaCoNGO) YARIDISHWA NA MCHAKATO WA UCHAZI NGAZI YA MIKOA NA WILAYA.

MWENYEKITI wa Kamati ya uchaguzi wa Baraza la  Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali  (NaCoNGO ) Wakili Fraviana Charles (kulia) akiwa na katibu Mtendaji wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga (kushoto) wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuelekea Uchaguzi Mkuu huo uliofanyika leo Julai 6,2021 Jijini Dar es Salaam.

MWENYEKITI wa Kamati ya uchaguzi wa Baraza la  Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali  (NaCoNGO ) Wakili Fraviana Charles Akizungumzia mchakato mzima wa uchaguzi 

katibu Mtendaji wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) juu ya mchakato mzima wa kuwapata viongozi wa Wilaya na Mikoa wa Baraza la  Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali  (NaCONGO ) na kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 8, Julai, 2021.

MWENYEKITI wa Kamati ya uchaguzi wa Baraza la  Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali  (NaCoNGO ) Wakili Fraviana Charles (kulia) akiwa na katibu Mtendaji wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga (kushoto) wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuelekea Uchaguzi Mkuu huo uliofanyika leo Julai 6,2021 Jijini Dar es Salaam.

MWENYEKITI wa Kamati ya uchaguzi wa Baraza la  Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali  (NaCoNGO ) Wakili Fraviana Charles (kushoto) akijadiliana jambo na Meneja Idara ya Mahusiano na Maendeleo wa (FCS) Nasim Losai.

Na: Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM.

MWENYEKITI wa Kamati ya uchaguzi wa Baraza la  Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali  (NaCONGO ) Fraviana Charles ametanga kuwa julai 8 utafanyika uchaguzi ngazi ya Taifa wa baraza hilo.hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa chaguzi ngazi ya Wilaya ,mikoa na mashirika.
Amesema kuwa Katika chaguzi za ngazi za Wilaya ,mikia na mashirika yamefanyika kwa mafanikio makubwa na kazi kubwa iliyobaki ni kuchagua viongozi ngazi ya Taifa nakwamba mkutano huo utafanyika Katika ukumbi wa Royal Village Jijini Dodoma.

Fraviana ameyasema hayo leo mbele ya waandishi wa habari ambapo amesema kuwa yeye Kama mwenyekiti Jukumu lake kubwa ni kuratibu na kusimamia uchaguzi wa Baraza la Taifa Mashirika yasiyokuwa yaserikali .

Amesema Baraza litakalo undwa litakuwa wawakilishi au wajumbe 30 kati ya hao wajumbe 26 kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na mjumbe mmoja kutoka kila mkoana wajumbe wanne watachaguliwa kutoka Katika Makundi maalum.

Amefafanua kuwa Makundi hayo ni pamoja na mashirika ya kimataifa ,watu wenye ulevmavu na watoto pamoja na Vijana .ambapo pia ametumia mkutano huo na waandishi wa habari kutoa taarifa ya matokeo ya uchaguzi wa baraza la Taifa la mashirika yasiyoyaserikali  Katika ngazi ya Wilaya uliofanyika Juni 26 2021.

Mwenyekiti Fraviana amesema kwa ujumla mchakato wa uchaguzi wa wajumbe wa NaCONGO Katika ngazi ya Wilaya ,Mikoa na wa Makundi maalumu ulifanyika kwa mafanikio makubwa mpaka kufikia hatua ya kupata rasmi wajumbe wote wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali( NaCONGO ) 

“Tunatarajia uchaguzi Katika ngazi ya Taifa utafanyika pia kwa ueledi na mafanikio makubwa ili tuweze kupata viongozi wa baraza jipya yaani Mwenyekiti ,Katibu mkuu ,pamoja na mweka wa Baraza.”amesema Fraviana.
Amefafanua kuwa baada ya uchaguzi Julai nane siku inayofuata Julai tisa wataapishwa viongozi wapya wa kitaifa na Julai 10 viongozi wapya watakabidhiwa nyaraka na ofisi kutoka kwa uongozi waliomaliza muda wake .

Akizungumzia uchaguzi wa ngazi za Wilaya ,Mikoa na mashirika katibu Mtendaji wa kamati ya uchaguzi ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa FCs amesema Katika mchakato wa uchaguzi huo uliopita changamoto zilikuwepo lakini wanashukuru wamemaliza salama na Sasa wanakwenda kumaliza kazi Katika ngazi hiyo ya Taifa.

Mwisho.
Previous articlePURA YAJIPANGA KUTANUA WIGO WA KUWAFIKIA WADAU WA SEKTA YA MAFUTA NA GESI NCHINI.
Next articleDKT.GWAJIMA AWATAKA WANANCHI KUZINGATIA TARATIBU WAKATI WA KUCHUKUA MIILI YA MAREHEMU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here