Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda (kulia) akimimina Kahawa kwenye kikombe cha Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (kushoto) kuashiria uzinduzi rasmi wa siku ya Kahawa kwenye maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam. |
Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda (kushoto) akimimina Kahawa kwenye kikombe cha Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Prof. Aurel Kamuzola wakati wa uzinduzi huo. |
Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akizungumza na wadau mbalimbali wa Kawaha (hawamo pichani) alipokuwa akitoa hotuba yake kwenye uzinduzi huo. |
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa siku ya kahawa kwenye maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam. |
Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa Tanzania Priscus Kimaryo Akizungumza na hadhara hiyo wakati wa kumkaribisha waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo kwenye uzinduzi huo. |
Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Tanzania Prof. Aurela Kamuzola akizungumza alipokuwa akihitimisha hafla hiyo kwa kutoa neno la shukrani. |
Mdau wa zao la Kahawa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya AMIMZA LTD Amir Hamza akizungumzia hafra hiyo namna ilivyofana na wao kama wadau kuweza kupata fursa ya kushiri. |
Mkurugenzi Mkuu Balozi Edwin Rutageruka awali akizungumza kuwatambua na kuwakaribisha wageni mbalimbali kwenye uzinduzi huo. |
Mtaalam wa Kahawa kutoka Bodi ya Kahawa akionesha Mashine Maalum ya kusagia Kahawa wakati wa ziara fupi ya Mgeni rasmi kupita kuijionea namna mMashine hiyo inavyofanyakazi. |
WAZIRI wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa zao la Kahawa hapa nchini limekua kwa kiasi kikubwa na kufanya Watanzania wengi kupenda kunywa kinywaji hicho.
WAZIRI Mkenda amesema hayo wakati wa uzinduzi wa siku maalum ya Kahawa nchini kwenye maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa wataendelea kushikamana na Bodi ya Kahawa kama ilivyo kwa bodi nyingine kwani kuna sehemu wakulima wameshaanza kukata tamaa wanaona hailipi.
“Nampongeza ndugu yangu Amir Hamza Kahawa ya Amimza utaikuta madukani Nairobi inauzawa, tungependa kuona Kahawa yetu ina sheheni kwenye masupamaketi ya Afrika Kusini, Angola, Namibia, Botswana, Zimbabwe, Tunisia tuende hadi China, amesema.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Tanzania,Prof. Aurelia Kamuzora amesema kuwa kampeni ya unywaji wa kahawa unafuata mnyororo wa thamani mkulima anavutwa na wanywaji kama hawatakuwepo kilimo cha kahawa kitakwama.
“Kunywa kahawa Kuna faida zake na kwa sasa kuna mtandao tafafhali nendeni mkatafute, kuna faida zaidi ya 100 za kinywa kahawa,”amesema Mwenyekiti huyo.
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa nchi ya Marekani ndio inayofanya mabadiliko mengi ya kidunia na ndio maana wanywaji Kwanza duniani.
Amesema kuwa inashauriwa asubuhi kunywa kikombe kimoja cha kahawa ili kuamsha ubongo uweze kufanya kazi vizuri na kwamba nchi za nje wanafanya hivyo lakini nchini walimaji wanakunywa kidogo.
Prof.Kamuzora ameeleza kuwa kunywa kahawa angalau kikombe kimoja kwa siku ili kusaidia ubongo kufanya kazi na kwamba unywaji ukiongezeka mkulima atafaidika.
“Namshukuru waziri wa viwanda na biashara Prof. Mkumbo kwa kufanya mazingira mazuri ya uwekezaji watu wanajitokeza kuchukua leseni za kuanzisha biashara za kahawa,” ameongeza kuwa, “tafadhali tafuteni leseni ili mfanye biashara tuvute kilimo kwani huwezi kutenganisha biashaa ya kahawa na kilimo “ ameongeza Prof. Kamuzora.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa bodi hiyo Priscus Kimaryo amesema zao la kahawa linashika nafasi ya pili duniani badala ya maji kwa kunywa.
Amesema kipindi cha nyuma kahawa ilikuwa inazalishwa kwenye nchi zinazoendelea na kutumiwa katika nchi hizo lakini kwa sasa hadi nchi zinazolima nazo zinatumia kahawa.
“Kwa mfano nchi ya Brazili ni ya kwanza kwenye uzalishaji na ni ya pili kwa unywaji wa kahawa duniani ukiachia Marekani, nchi zinazozalishwa zenyewe zina kunywa kahawa kwa Tanzanai utamaduni wa kunywa ulikuwa zaidi kwenye mikoa ya Pwani na visiwani Zanzibar,” amesema.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa hivi sasa asilimia kubwa ya unywaji upo kwenye vijiwe na kwamba Tanzania ina viwanda 28 vya kukaanga imetoka kwenye kuacha kukoboa na kwenda kwenye viwanda hivyo.
Amesema pamoja na uwepo wa viwanda hivyo uzalishaji Hali ya unywaji wa kahawa upo chini kwa wastani wa asilimia 7.
“Mkakati uliopo ni kufikia asilimia 15 ya tunachokizalisha, duniani hivi sasa ndio ambayo watu wake wanakunywa kahawa na haina matatizo,” amesema.
Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa kuna changamoto kubwa ya za mashine ikilinganishwa ma sekta ya chai mashine zake ni gharama na vifingashio pia.
“Changamoto nyingine ni kwa wale wanaotengeneza kahawa wapo wachache, tunaendelea kutoa elimu kama bodi kuhakikisha wanakuwa wengi “ amesema.
Pia amesema mkakati walionao ni kukuza unywaji w kahawa na kuwashauri wawekezaji wa vifungashio wa hapa nchini wawekeza kwenye utengebezaji was vifungashio hivyo kwani vingi vinatoka nje ya nchi.