Home ENTERTAINMENTS JUX KUKIWASHA KAHAMA NA VIUNGA VYAKE JULAI 30.

JUX KUKIWASHA KAHAMA NA VIUNGA VYAKE JULAI 30.

Picha ya Maktaba.

Mbwana Imamu ambaye ndio muandaaji wa Tamasha hilo kupitia kampuni yake ya ARBAB MB ENTERTAINMENT(katikakati) akitoa ufafanuzi kwenye mkutano na waandishi wa Habari kuhusu ujio wa Msanii Juma Jux katika Manispaa ya Kahama.

Na:Saimon Mghendi,Kahama

Msani wa muziki wa kizazi kipya nchini maarufu kama Bongo Flava, Juma Jux, anatarajiwa kufanya tamasha la muziki katika manispaa ya Kahama ifikapo julai 30 mwaka huu katika ukumbi wa African Lounge uliopo katika manispaa hiyo.

Akitoa ufafanuzi kwenye mkutano na waandishi wa Habari, Mkutano ambao umefanyika leo katika ukumbi wa African Lounge, katika Manispaa ya Kahama, Muandaaji wa Tamasha hilo kupitia kampuni yake ya ARBAB MB ENTERTAINMENT, Mbwana Imamu, amesema kuwa lengo kubwa lakumleta msanii huyo Kahama ni kuwaleta watu Pamoja sambamba na kutoa burudani.

Pia Mbwana Imamu alitaja kiingilio cha Tamasha hilo kuwa ni Tsh.10,000 na VIP Tsh.30,000 na kutumia fursa hiyo kutoa wito kwa wakazi wa Kahama na maeneo ya Jirani waweze kujitokeza kwa wingi katika ukumbi wa African Lounge ifikapo julai 30.

Kwa upande wake Event Meneja wa Ukumbi wa African Lounge Victor Joseph, amewahakikishia wapenzi wa burudani katika Manispaa ya Kahama na maeneo ya Jirani kuwa hali ya ulinzi ni asilimia mia moja.

Previous articleSERIKALI IMEFANYA MABORESHO YA MIUNDOMBINU KWA AJILI YA KUPIMA CORONA UWANJA WA NDEGE PROF: MAKUBI.
Next articlePROF. MKENDA AZINDUA SIKU MAALUM YA KAHAWA MAONESHO YA SABASABA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here