Home LOCAL NAIBU WAZIRI WA ELIMU AYAFUNGA RASMI MAONESHO YA 16 YA VYUO VYA...

NAIBU WAZIRI WA ELIMU AYAFUNGA RASMI MAONESHO YA 16 YA VYUO VYA ELIMU YA JUU LEO JULAI 31,2021

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Omary Kipanga (katikati) akipokelewa na wenyeji wake Makamu Mwenyekiti wa TCU na Makamu Mkuu wa Chuo cha kumbukumbu ya Hurbert Kairuki Prof. Charles Mgone (wa kwanza kushoto) na Katibu Mtendaji wa TCU Prof. Charles Kihampa (kulia) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam kufunga Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na (TCU) kwa siku sita.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Omary Kipanga (kushoto) akizungumza na Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi wa TCU Hilda Kawiche (kulia) alipofika kwenye Banda la Tume hiyo kupata maelezo ya namna wanavyofanya kazi zao. (wa ipi kushoto) ni Prof. Charles Kihampa Katibu Mtendaji wa TCU
Katibu Mtendaji wa TCU Prof. Charles Kihampa (kushoto) akimkabidhi Zawadi ya Vitabu Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Omary Kipanga,akizungumza alipomaliza ziara fupi ya kutembelea Banda la TCU.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Omary Kipanga,akizungumza wakati akifunga Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na TCU na kufanyika kwa siku sita katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.

Shamim Mdee Meneja Masoko na Uhusiano kwa Umma wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi PSTPB (mwenye fulana nyeusi) akiwa na Wakuu wa Taasisi za Elimu ya Juu wakifuatilia kwa karibu hotuba kutoka meza Kuu.


DAR ES SALAAM | Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Omary Juma Kipanga, leo ameyafunga rasmi Maonesho ya 16 ya Eimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yaliyokuwa yakifanyika kwa siku sita katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.

Katika hafla ya ufungaji wa maonesho hayo Naibu waziri huyo alifanya ziara ya kutembelea Mabanda ya Vyuo Vikuu na Taasisi Mbalimbali za Elimu ya Juu zilizoshiriki maonesho hayo na kujionea shughuli mbalimbali ikiwemo zoezi la udahili wa wanafunzi wapya wa mwaka wa kwanza uliofanywa na Taasisi hizo papo hapo.

Akizungumza wakati alipokuwa akitoa hotuba yake Naibu waziri Kipanga amezitaka Taasisi za elimu ya juu kutambua kwamba bado zinakazi kubwa ya kuongeza wataalam wa kiwango cha ujuzi wa juu na kati kwani bado taifa halina wataalam wa kutosha katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo wenye kiwangi hicho cha elimu hususani katika masuala ya Sayansi na Teknolojia nakwamba ukuaji wa uchumi na mafanikio katika Sekta ya uzalishaji inategemea kwa kiasi kikubwa uwepo wa rasilimali watu wenye ujuzi na maarifa ya kubuni na kuendeleza Teknoloji mbali mbali na kutatua changamoto zinazokabili jamii yetu na taifa kwa ujumla.

Amesema, kwa takwimu za 2016 zinaonyesha watu wenye ujuzi wa juu ni asilimia 3.3 huku wenye ujuzi wa kati ni asilimia 17, kitu kinachoonyesha kwamba taasisi zetu za elimu ya juu bado zinakazi kubwa ya kuongeza wataalamu wa kiwango cha ujuzi wa juu na wa kati.

“Ukuaji wa sekta zingine za kiuchumi hauwezi kuwa na mafanikio yaliyokusudiwa pasipokuwepo na mchango wa elimu ya juu sayansi na Teknolojia, ili kudumu na kufikia uchumi wa kati wa juu nchi lazima iwe na watu wenye ujuzi wa juu kwa asilimia 12 na ujuzi wa kati kwa asilimia 26.

Naibu waziri Omary pia amezitaka taasisi za elimu ya juu za serikali na binafsi kuweka mipango itakayoongeza idadi ya wahitimu wa Vyuo Vikuu wenye ujuzi na ushindani katika soko la ajira na kuongeza kuwa serikali inaendekea kuboresha Vyuo mbalimbali nchin ili viweze kutoa elimu bora ya kiushindani ndani na nje ya nchi.

Aidha amezihimiza taasisi za elimu ya juu kuwekeza zaidi katika tafiti na ubunifu ambapo katika kipindi Cha miaka mitani ijayo serikali imedhamiria kuwekeza katika sekta ya ubunifu na utafiti ili nchi iweze kupata bunifu na tafiti zenye kutatua changamoto za wananchi na kukuza uchumi wa nchi.

Aidha ametoa wito kwa TCU kuongeza jitihada katika udhibiti wa ubora na kufanya maboresho stahiki ili kuhakikisha kuwa vyuo vikuu vinatoa wahitimu bora na wenye uwezo wa kuhimili ushindani katika soko la ajira.

Amesema kuwa serikali itaendelea kuenzi ubia na ushirikiano baina na sekta ya umma na sekta binafsi katika utoaji wa elimu ya juu japa nchini kwa kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wawekezaji bila kuathiri ubora wa elimu

Naye Katibu Mtendaji tukoka Tume ya Vyuo Vikuu Prof Charles Kihampa amesema kupitia maonesho hayo wananchi wameweza kujifunza na kuona yanayofanywa na vyuo vya elimu ya juu ikiwemo namna ya kujiunga na vyuo ambapo katika maonesho jumla ya wahitimu zaidi ya elfu hamsini na nne wameweza kutuma maombi ya kujiunga na elimu ya juu ikiwa dirisha la udahili lilishafunguliwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here